1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA : Waasi wagoma kusalimisha silaha

15 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Fk

Waasi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamesema hapo jana hawatosalimisha silaha zao bila ya kuwa na mazungumzo licha ya onyo la serikali la kutaka wafanye hivyo ama sivyo watakabiliwa na shambulio jipya la serikali.

Serikali ya imewapa vikosi vya waasi chini ya Generali wa Kitutsi Laurent Nkunda hadi leo kusalimisha silaha venginevyo kujiunga na jeshi nchini ya mchakato wa kuwajumuisha jeshini au kurudi kwenye maisha ya kiraia.

Serikali imegoma kuzungumza na waasi hao ambao imekuwa ikipambana na vikosi vya serikali katika mkoa wa mashariki wa Kivu ya Kaskazini kwa wiki nzima.

Msemaji wa Nkunda amesema hawatosalimisha silaha wakati wanajeshi wa serikali wakiendelea kuwashambulia na kwamba watajibu mapigo kwa shambulio lolote lile.