1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA : Waasi waongezewa muda kujiunga jeshini

16 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7FX

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imeongeza muda wa mwisho kwa waasi wa Generali Laurent Nkunda kujiunga la jeshi la kawaida wakati mapigano yakizuka upya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Vikosi vya serikali na vile vya Nkunda mara kwa mara vimekuwa vikipambana kwenye mkoa wa Kivu kaskazini kwa takriban mwaka mmoja sasa.

Waziri wa ulinzi Chikez Diemu amekaririwa akisema kwamba wametowa siku 21 zaidi kwa wanajeshi waliogeuzwa mateka na mhalifu Nkunda kujiunga na mchakato wa kujumuishwa jeshini na kurudi kwenye maisha ya kawaida ya kijeshi.