1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA: Wakazi nchini Kongo wakimbia mapigano

26 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCpH

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo,vikosi vya serikali katika mji wa Sake mashariki mwa nchi vimeshambuliwa na wapiganaji wanaomuunga mkono Laurent Nkunda alieasi.Msemaji wa jeshi la Kongo amesema,vikosi vya serikali vimewazuia waasi walio tiifu kwa Laurent Nkunda.Kwa sababu ya mapigano yaliyozuka,zaidi ya watu 10,000 wameukimbia mji huo ulio kilomita 20 magharibi ya mji wa Goma.Kwa mujibu wa msemaji wa majeshi ya Umoja wa Mataifa,wanajeshi 2 wa serikali pia waliuawa.Duru zingine zinasema,si chini ya watu 15 walijeruhiwa ikiwa ni pamoja na raia 8.Hali ya machafuko imebakia katika maeneo ya mashariki nchini Kongo,licha ya vikosi vya amani vya Umoja wa Mataifa kuwepo katika eneo hilo na mkataba wa amani kutiwa saini mwaka 2003.Rasmi mkataba huo wa amani,umemaliza vita vya miaka mitano nchini humo.