1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA.Bemba akubali kushindwa

29 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCoV

Kiongozi wa kundi la zamani la waasi katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Jean Pierre Bemba amekubali kushindwa katika uchaguzi wa rais uliomalizika baada ya kesi alyowasilisha katika mahakama kuu kupinga matokeo ya uchaguzi kutupiliwa mbali.

Bemba amesema kwa ajili ya amani ya nchi yake ataendeleza juhudi za kutafuta mabadiliko katika upande wa upinzani wenye nguvu kwa manufaa ya nchi hiyo.

Uchaguzi wa mwezi uliopita nchini Kongo umetia kikomo cha mapigano ya miaka mitano yaliyoikumba jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo tangu mwaka 2003.

Wachunguzi wa kimataifa wamesema kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa haki na uwazi.