1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA:Makubaliano ya kusimamisha vita yafikiwa

7 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBS5

Umoja wa mataifa umesema kwamba umefanikisha makubaliano ya kusimamisha mapigano kati ya vikosi vya serikali na kikosi kinachomtii jenerali muasi Laurent Nkunda.

Makubaliano hayo yamepatikana kufuatia mapigano ya zaidi wiki moja yaliyozuka huko mashariki mwa Kongo.

Makubaliano hayo ya kusimamisha mapigano yalifikiwa katika mji wa mashariki ya Kongo wa Sake.