1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA:Mapigano Ituri kati ya waasi wa FNI na majeshi ya serikali

1 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCWJ

Mapigano yameripotiwa kutokea kati ya majeshi ya serikali na waasi katika eneo la kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo katika operesheni dhini ya kiongozi mmoja wa waasi.Kwa mujibu wa taarifa hakuna vifo au majerihu wowote walioripotiwa.

Kulingana na kiongozi wa kundi la waasi hao Jenerali Vainqueur Mayala aliyeko eneo la Ituri,milio ya risasi ilisikika asubuhi hii karibu na eneo la Fataki liilokaribu na mji wa Bunia.Majeshi ya serikali ya Kongo FARDC yalipambana na waasi ili kuwafurusha katika maeneo yao.

Umoja wa Mataifa ukishirikiana na majeshi hayo ya serikali walianzisha mwezi jana operesheni ya kusalimisha waasi wa eneo hilo kwa kushika doria.Mpaka sasa silaha kadhaa zimekamatwa na wanajeshi hao.Mapigano hayo yanatokea wakati hali ya wasiwasi inatanda eneo la Ituri ambako majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa mataifa MONUC yanazidisha shughuli zake za kijeshi katika eneo hilo lili kuunga mkono jeshi la Kongo kupambana na waasi.

Tangu mwezi Julai mwaka jana Karim aliyekuwa katika kundi la waasi wa Nationalist and Integrationist Front FNI anaahidi kusalimisha wapiganaji wake ili kuweza kusamehewa na kujiunga na jeshi la serikali la FARDC katika cheo cha Kanali ambacho ashapewa.

Karim analaumiwa kuhusika na vitendo vya uhalifu wa kivita vilevile kusafirisha bidhaa kimagendo hadi nchi jirani ya Uganda.Yeye ndiye kiongozi wa mwisho anayeshikilia kuendelea na uasi.Mpaka sasa wapiganaji alfu 15 wameweka silaha zao chini tangu mwaka 2005 ilipoanza shughuli hiyo ya kurejesha waasi katika maisha ya kawaida kuanza.