1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA:Sita watuhumiwa kutupa taka za sumu mtoni

10 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CBKI

Watu sita wamekamatwa nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya kongo kutokana na kutuhumiwa kutupa taka za sumu katika mto.

Habari zinasema wahusika walitoa agizo la kutupa tani kadhaa za taka hizo kwenye mgodi wa zamani wa madini ya uranium.

Lakini baadhi ya watu waliokua na dhamana ya kuhakikisha utaratibu salama wa kutupa mabaki hayo pia ni miongoni mwa waliokamatwa.

Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo inawashauri wananchi wa mji wa Likasi kutotumia maji kutoka mto Mura