1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA:Waasi wa Nord Kivu watoa madai mapya

25 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Cn

Waasi katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wametoa madai mapya hii leo kabla kujisalimisha jambo linalokwamisha shughuli ya kuwasajili katika jeshi la serikali.Mamia ya waasi wamekusanyika katika kambi moja maalum ya Umoja wa mataifa kwenye mkoa wa Kivu ya Kaskazini kabla kusajiliwa katika jeshi la serikali.Jenerali muasi Laurent Nkunda anayepambana na majeshi ya serikali tangu mwezi Agosti aliahidi kuwaruhusu wapiganaji wake 500 kujiunga na jeshi la serikali.

Hatua hiyo inaashiria juhudi za kiongozi huyo wa waasi za kutaka kujadiliana na serikali badala ya kushambuliwa na majeshi ya serikali.Hakuna wapiganaji wowote waliofika katika mji wa Kirolirwe hapo jana ila Jenerali Bwambale Kakolele aliye kamanda wa ngazi za juu katika kundi la Nkunda alishaagizwa kufika katika kambi hiyo.

Jenerali muasi Laurent Nkunda ameendesha mashambulizi mara mbili dhidi ya serikali mwaka 2004 na kuondoa wapiganaji wake kwa mara ya pili katika jeshi la taifa mwezi Agosti.Kiongozi huyo wa waasi ameahidi kuwaruhusu wapiganaji wake kujiunga na jeshi la serikali ila mpaka sasa bado hilo halijatimizwa.