1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinyang'anyiro cha Premier League chapamba moto

24 Machi 2014

kinyang'anyiro cha taji la ligi kuu ya England - Premier League kimepamba moto, huku kukionekana kuwa ni mbio za farasi watatu: Chelsea, Manchester City na Liverpool

https://p.dw.com/p/1BV3X
Fußball Premier League Chelsea Arsenal
Picha: Getty Images

Mchuano wa utani wa jiji la Manchester hapo kesho 25.03.2014 ndio utakaokuwa kilele cha mechi tano zitakazochezwa katikati ya wiki hii katika Premier League. Manchester United ambao wako nyuma ya Chelsea na pengo la points 18, hawana ndoto tena za kuhifadhi taji la ligi, lakini wanalenga kuwasimamisha nambari tatu Manchester City kuwapiku kama mabingwa.

Baada ya kunyukwa vibaya na mahasimu wao magoli manne kwa moja mwezi Septemba, United wana faida ya kucheza nyumbani Old Trafford na wanashuka dimbani wakiwa na matarajio makubwa baada ya ushindi wao dhidi ya Olympiakos uliowakatia tikiti ya robo fainali ya Champions League.

Wayne Rooney ataongoza safu ya mashambulizi ya Man United dhidi ya Manchester City
Wayne Rooney ataongoza safu ya mashambulizi ya Manchester United dhidi ya Manchester CityPicha: picture alliance / empics

Kisha wakapata ushindi wa mabao mawili kwa sifuri dhidi ya Westham ili kumwondolea shinikizo kocha wao David Moyes. City wako nyuma ya Chelsea na tofauti ya points sita lakini wana mechi tatu za kuchezwa pamoja na idadi nyingi ya magoli na wanaweza kwenda kileleni kamawatashinda mechi mbili kati ya hizo tatu.

Liverpool wamejiunga katika kinyang'anyiro hicho na wanalenga kuendeelza shinikizo dhidi ya viongozi Chelsea watakapopambana na Sunderland uwanjani Anfield. Arsenal watakabana koo na Swansea City hapo kesho, nao Newcastle wawakaribishe Everton, abao wanatafuta kibali cha kucheza katika Europa Legaue.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Yusuf Saumu