1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiongozi wa Ghana aiomba radhi Nigeria

Sylvia Mwehozi
24 Juni 2020

Kiongozi  wa  Ghana  ameomba  radhi kwa  Nigeria kuhusiana  na  kuvunjwa  kwa  jengo  la  ubalozi  wake mjini  Accra, ofisi  ya  rais  wa  Nigeria  imesema

https://p.dw.com/p/3eGmx
Afrika Ghana - Nana Akufo-Addo gewinnt Präsidentschaftswahl
Picha: picture-alliance/dpa/C. Thompson

Kiongozi  wa  Ghana  ameomba  radhi kwa  Nigeria kuhusiana  na  kuvunjwa  kwa  jengo  la  ubalozi  wake mjini  Accra, ofisi  ya  rais  wa  Nigeria  imesema.

Rais Nana  Akufo-Addo wa  Ghana jana  alizungumza  na rais Muhammadu Buhari  wa  Nigeria, ameeleza kuomba kwake  radhi  kutokana  na  kuvunjwa  kwa  jengo  hilo katika  eneo  la  ubalozi  wa  Nigeria  mjini Accra, Ghana, imesema  taarifa  kutoka  ofisi  ya  rais jana.

Akufo-Addo  pia  ameamuru  uchunguzi  kuhusu tukio  hilo, taarifa  imesema, na  kuongeza  kuwa  baadhi  ya washukiwa  wamekamatwa  na  watashitakiwa.

Watu wenye  silaha  wanaripotiwa  kuingia  katika  eneo  la ubalozi  huo  wa  Nigeria mjini  Accra  siku  ya Ijumaa kuelekeza  matrekta  kuvunja  jengo ambalo  lilikuwa  bado linajengwa. Waziri  wa  mambo  ya  kigeni  wa  Nigeria Geoffrey Onyeama siku  ya  Jumatatu alimuita  balozi  wa Ghana  Iva Denoo mjini  Abuja  kudai kupata  maelezo kuhusiana  na  tukio  hilo.