1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kipa wa Taifa wa Ujerumani Robert Enke ajiua ?

11 Novemba 2009

Sera za serikali ya Kanzela Merkel zaelekeza wapi ?

https://p.dw.com/p/KTpG
Marehemu Robert EnkePicha: DPA

Maoni ya wahariri wa magazeti ya leo ya Ujerumani, yamejishughulisha mno na visa 2: Kifo cha kustusha cha kipa wa timu ya Hannover 96 na wa timu ya Taifa ya Ujerumani ,Robert Enke, aliejiua jana jioni katika kivuko cha treni.Mada ya pili, ni hotuba ya Kanzela Angela Merkel katika Bundestag-Bunge la Ujerumani, mjini Berlin ambamo alichambua sera za serikali yake mpya ya muungano :

Akianza na uchambuzi wa Badische Nueste Nachrichten, gazeti hilo laandika:

"Kanzela Merkel ,akiwa ubavuni mwa mshirika wake wa kiliberali serikalini (FDP) alionesha mwenye ujasiri zaidi na asemae kwa uwazi zaidi kuliko alipoongoza serikali ya muungano wa vyama vikuu iliopita.Hata Kiongozi mpya wa upinzani Bungeni wa chama cha SPD,Bw.Steinmeier, amebanika ni msemaji wa kusisimua na wa nguvu za hoja.Usuhuba wa watu hao 2 ambao vyama vyao uliokuwa nao mnamo miaka 4 iliopita jana waliouzika ."

Gazeti la Flensburger Tageblatt lauliza ni kitu gani hasa alichotangaza jana bungeni Kanzela Angela Merkel ? Likaongeza:

"Walipakodi katika kipindi hiki cha msukosuko wa fedha, watatozwa mabilioni ya fedha .Kizazi kichanga hakitaweza kulala usingizi kwa mzigo mkubwa wa madeni kinaojitwika serikali na wastaafu kwa kupungua mapato yao ya pencheni itwabidi kuomba dua kuwa bei za vitu, hazitapanda mno.Kile lakini alichotangaza kiongozi huyo wa serikali ni hiki: Matatizo hayo yatazidi kwanza kuwa makubwa kabla kupungua. Hizo ni salamu gani kuwapa wanannchi kwa siku zinazofuata ?"

Ama gazeti la Financial Times Deutschland, limegundua hapo jana Bungeni kwamba, kulitanda hali ya kuvuta pumzi tangu kwa wabunge hata kwa wasikilizaji jukwaani baada ya kuondoka kwa serikali ya mseto ya vyama vikuu.

Financial Times laongeza:

"Wabunge wa vyama mbali mbali walioonekana huru wakipiga makofi au wakiwazomea wanzao ama upande wa serikali au wa Upinzani,kwavile, hawajikuti tena wamefungwa pingu kubidi kufuata msimamo wa vyama vyao kinyume na ilivyokuwa wakati wa serikali ya muungano wa vyama vikuu...."

Kuhusu kifo cha kustusha jana jioni cha kipa wa Hannover 96,klabu ya bundesliga na wa Taifa wa timu ya Ujerumani, Robert Enke, gazeti la Hamburger Morgenpost laandika:

"Robert Enke ,mlinda lango stadi kabisa,aliumaliza umri wake wa miaka 32 katika kivuko cha gari-moshi.Kujiua mwenyewe huko kunazusha kitandawili: Kwani, ikibainika alikwisha sahau majonzi ya kifo cha mwanawe mdogo .Hakika lakini, Enke alikuwa na matatizo makubwa ya afya,hatahivyo, kurejea tena kuwa kipa wa Taifa, mlango kwake ulikuwa bado wazi.Kwanini basi alijiua ?

Kwa jicho la nje yadhihirika kana kwamba , stadi mwengine wa Bundesliga,hakuweza kuvumilia vishindo vya Ligi hiyo ya Ujerumani.Kwani, kisa chake hiki kinakumbusha kile cha stadi mwengine wa Taifa: Sebastian Deisler, ambae alitoroka jumba la wendawazimu la klabu ya Bayern Munich.......Bundesliga ya wachezaji wa malipo, kufuatia kifo cha Robert Enke,yafaa sasa kukaa chini na kujiuliza: ilikuaje, misiba kama hii ya wachezaji inatokea ? "

Mtayarishi: Ramadhan Ali /DPA

Mhariri:Abdul-Rahman