1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kipchoge Keino atimiza miaka 75 ya kuzaliwa

16 Januari 2015

Alikuwa mmoja wa wanariadha wa kwanza wa Kenya kuwika katika jukwaa la kimataifa na tangu wakati huo, amebakia kuwa nguli. Leo Jumamosi (17.01.2015) Kipchoge Keino anafikisha umri wa miaka 75

https://p.dw.com/p/1ELoD
Kenia Läufer Kipchoge Keino
Picha: AP

Kipchoge Keino, mmoja wa wakimbiaji wa kwanza wa miujiza nchini Kenya, ni shujaa ambaye amefika katika anga za mbali na leo, Rais huyo wa Kamati ya Kitaifa ya Olimpiki – NOCK anaadhimisha miaka 75 ya kuzaliwa.

Alishinda dhahabu katika michezo ya Olimpiki akiwa na matatizo ya figo, amewapa hifadhi zaidi ya watoto mayatima 100 na anajihusisha kwa kiasi kikubwa katika vita dhidi ya matumizi ya dawa za kuongeza nguvu. Keino ndiye Mwafrika wa kwanza kuvunja frekodi ya ulimwengu na mnamo mwaka wa 2012, akaongezwa katika orodha ya IAAF ya wanariadha nguli.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Yusuf Saumu