1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kipi kimembakisha Merkel madarakani muda mrefu?

Sekione Kitojo
13 Septemba 2017

Ndani na nje ya kampeni, Kansela Angela Merkel hudhihirisha kipaji cha kupima upepo na kuuelekeza kwake dhidi ya wapinzani wake. DW inaangalia baadhi ya mbinu ambazo zimemsaidia kubakia madarakani kwa muda mrefu zaidi.

https://p.dw.com/p/2jrxu
Deutschland | Bundestagswahl 2017 | Wahlplakat CDU
Picha: picture-alliance/R. Goldmann

"Nikiangalia  ni vituo  vingapi vya  nishati  ya  nyuklia  vinajengwa  duniani  kote," kansela  amesema  alisema  mwaka  2008, "itakuwa ni  aibu  kubwa  iwapo tutaondoka  kutoka  sekta  hii."

Lakini  hicho  ndio alichofanya haswa  Angela  MerkeL mwaka 2011. Kutokana na  maafa  ya  Fukushima, alibadilika  haraka  na kutaka  kufikishwa  mwisho wa nishati ya nyuklia  nchini  Ujerumani.

Hili lilikuwa  suala  la  msingi  kwa  chama  cha  Kijani  kwa  miongo  kadhaa. Kinyume na matamshi  yake  ya  hapo  awali, Merkel , ambaye  ni mtaalamu wa masuala  ya  fizikia, alisema  wakati  huo: "Hatari ya  nishati  ya  atomic haiwezi kudhibitiwa  kwa  usalama."

Katika  wakati  kama  huo ,  kutumikia  jeshi kwa mujibu  wa  sheria  kulifikishwa  mwisho, licha ya chama  chake cha  kihafidhina  cha Christian Democratic Union (CDU) kutoridhia maamuzi  hayo. Vijana  wengi wa  Ujerumani wanapendelea  kutumikia  jeshi, hata  hivyo, ni msimamo  ambao  Merkel  hakuufumbua  macho. Kutokana  na  hisia  mchanganyiko  za  Wajerumani  kuhusiana  na  mada  hiyo, uandikishwaji  jeshini  kwa  mujibu  wa  sheria  ulisitishwa  tu badala  ya  kuondolewa  kabisa. 

Kwa mshangao wa wahafidhina wengi  wenye  msimamo  mkali katika chama chake  cha  kihafidhina  cha  CDU, Merkel amekielekeza  chama  chake  katika  sera za  siasa  za  wastani wakati  linapokuja  suala  la  sera  za  familia. Msimamo  wa  asili wa Christian Democrats  wa "baba analeta  nyumbani  mkate na  mama  anauweka  mezani " ulitupiliwa  mbali  baada  ya  uamuzi wa kutoa elimu kamili kabla  ya  watoto  hawajaanza  shule  wakiwa  na  umri  wa  miaka  mitatu  na  chini  ya  hapo, na  mtazamo  mpya kabisa  wa  hali  halisi  ya  biashara  na  jamii.

Chama  cha  mrengo  wa  kushoto  kimekuwa  kikiongoza  mabadiliko  haya, lakini  walikuwa  ni  wahafidhina  ambao  uungaji  wao mkono  ulisukuma sera  hiyo  kupita  katika msitari.

Suala  hili pengine  zaidi  ya  mengine , linaakisi  unyumbulifu  wa  kisiasa  wa  Merkel. Mapema majira  ya  joto , uchunguzi  wa maoni  uliotolewa  na  kituo  cha  taifa  cha  televisheni  cha  ZDF  ulionesha  kwamba  asilimia  73 ya  Wajerumani na  asilimia  64 ya wapiga kura  wa  chama  cha  CDU, wanapendelea  kuwapatia  mashoga  haki  ya  kuoana  kama  watu wengine  wanaopendelea kuoana  kati  ya  mke  na  mume.  

Merkel  alikuwa  kila  mara  dhidi  ya  suala  hilo, licha  ya  vyama  vingine , ikiwa  ni  pamoja  na  chama  kinachounda  serikali  ya mseto  pamoja  na  chama  cha  CDU, chama  cha  Social Democratic (SPD), na  kile  cha  kijani wakifanya suala  hilo  kuwa  sharti la  kwanza  kwa  kuunda  muungano  wa  serikali  baada  ya  uchaguzi  mkuu  wa  hapo  Septemba  24.

Merkel  alibadili msimamo  wake  kiasi  siku  chache  baadaye, na  kuruhusu wabunge kupiga  kura  kwa  mapenzi  yao, badala  ya kufuata  msimamo  wa  chama.

Usawa  wa  ndoa  ulipitishwa  Juni 30. Merkel alipiga  kura  kupinga  mswada  huo , na  kujiwekea nafasi  ya  uwezo  wakati  huo huo kuliondoa  suala  hilo  kutoka  katika  uchaguzi  ujao, na  hatimaye  mazungumzo  ya  kuunda  serikali, wakati  bado  akikihakikishia chama  chake  cha  kihafidhina  kwamba  hajasalim amri kwa  msimamo  wake  wa asili.

Mwandishi: Volker Wagener / ZR / Sekione  Kitojo

Mhariri: Yusuf, Saumu