1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kisukari: Ugonjwa hatari unaodharauliwa

10 Juni 2011

Watu wengi hawajali kwamba Kisukari ni maradhi yanayoweza kuwapata wakati wowote ule kutokana na sababu kadhaa, zikiwamo za aina ya vyakula wanavyotumia na mtindo wao wa maisha walionao.

https://p.dw.com/p/11YMY
Upimaji wa afya
Upimaji wa afyaPicha: Fotolia/Alx

Hasa katika mataifa ya Mashariki ya Afrika, ikiwemo Tanzania, ugonjwa wa Kisukari hautiliwi maanani. Wengi hupatwa na matatizo yanayoletwa na ugonjwa huo na kuselelea nayo kwa miaka kadhaa, kabla hawajaenda hospitali.

Katika makala hii ya Afya, Rose Athumani, anaangalia tatizo la ugonjwa wa Kisukari na namna ambavyo watu wanaweza kujikinga nao.

Mtayarishaji/Msimulizi: Rose Athumani
Mhariri: Othman Miraji