1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ng'ombe atabaki kuwa mnyama mkubwa pekee

Veronica Natalis
20 Aprili 2018

Ripoti kuhusu utafiti wa kisayansi wa wanyama iliyotolewa mwaka huu, inaonya kuwa kuna kitisho cha kupotea kwa wanyama wakubwa duniani kama vile twiga, boko na tembo na hivyo kumuacha ng'ombe pekee atakayebakia

https://p.dw.com/p/2wQCu
DW eco@africa
Picha: DW

Ripoti inayoongelea utafiti wa kisayansi wa wanyama iliyotolewa mwaka huu, inaonya kuwa kuna kitisho cha kupotea kwa wanyama wakubwa duniani kama vile twiga, boko na tembo na hivyo kumuacha ng'ombe kuwa mnyama pekee mkubwa atakayebakia duniani miaka mia moja ijayo. Utafiti huo unabainisha kuwa ongezeko la watu katika maeneo mbalimbali duniani kunachangia kitisho hicho kutokana na shughuli za kibinaadamu.

Utafiti huo wa kisayansi umebainisha kuwa kuenea kwa binadamu duniani hasa kutoka bara la Afrika miaka zaidi ya elfu moja iliyopita kunatishia uwepo wa wanyama wakubwa na kumfanya ng'ombe kuwa mnyama mkubwa pekee aliyebaki duniani katika muda wa karne chache zijazo. Kuenea na homoni za binadamu wa kale wenye spishi kama za Neanderthals kutoka Afrika kunasababisha kupotea kwa wanyama hao wakubwa.

Spishi za homoni za binadamu wakale zahusishwa

Felisa Smith kutoka Chuo Kikuu cha New Mexico nchini Marekani aliwaambia waandishi wa habari wa shirika la Reuters kwamba, ripoti ya kisayansi iliyochapishwa katika tovuti moja huko nchini Marekani inaonesha kuwa kuna mfano wa wazi sana wa ukubwa wa uharibifu unaofuatia uwepo wa homoni kutoka nje ya bara la Afrika.

Wanaadamu waliwawinda wanyama wakubwa kwa ajili ya kupata nyama na wakati viumbe vidogo kama vile panya vilitoroka na hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya kuchunguza mwenendo wa wanyama zaidi ya miaka elfu kumi na mbili na mia tano. 

Huko Amerika ya Kaskazin, kwa mfano, sehemu kuu ya ardhi, wanyama kwa ajili ya nyama wamepungua uzito mpaka kufikia kilogramu saba nukta sita kutoka uzito wa kilogramu 98 baada ya binadamu kuwasili. Timu ya utafiti kutoka Marekani iliandika kwamba kama hali hii ikiendele,a mnyama mkubwa pekee atakayebaki katika miaka mia moja ijayo ni ng'ombe wa kufugwa mwenye uzito wa kilogram 900, na hiyo inamaanisha kwamba viumbe vingine ambavyo ni wanyama wakubwa kama vile twiga, tembo na viboko watapotea. 

Letztes männliches Nördliches Breitmaulnashorn der Welt gestorben
Picha: picture-alliance/Photoshot/S. Ruibo

Faru pekee mweupe duniani afariki nchini Kenya.

Mwezi wa tatu mwaka huu, faru mweupe wa mwisho kabisa duniani alikufa nchini Kenya. Lakini tafiti zingine zinanaonesha shaka juu ya kuendelea kufa kwa wanyama wengine kwa sababu ya juhudi za hifadhi ya kuzuia vitisho kwa wanyamapori kama vile mabadiliko ya hali ya hewa, kupotea kwa misitu, uchafuzi wa mazingira na ukuaji wa miji. 

Thomas Brooks, mwanasayansi mkuu kutoka muungano wa kimataifa wa uhifadhi wa viumbe asilia, IUCN, ambaye hakuhusika katika utafiti huo, aliwaambia waandishi wa habari wa shirika la Reuters kuwa utafiti mwingine unaonesha kwamba wanyama wakubwa kama tembo wanaweza kufaidika katika maeneo yaliyohifadhiwa kuliko wanyama wadogo. 

Orodha ya aina za wanyama zilizohifadhiwa na ICUN inawataja wanyama hao wa porini wenye ukubwa unaolingana na ng'ombe kama vile nyati wa Afrika, kuwa sasa wapo hatarini kupotea. 

Utafiti wa kisayansi pia huhusisha wanyama wa baharini kama vile nyangumi wa buluu kiumbe kikubwa zaidi cha baharini kilichobaki. 

"Mimi ningependa kusema kwamba matumaini yangu hayawezi kupotea kwa sababu ninawapenda tembo, lakini idadi ya wanyama wengi wa ardhi ilishuka." Anasema Thomas Brooks.

Mwandishi: Veronica Natalis/Reuters
Mhariri: Mohammed Khelef