1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kitisho cha machafuko Msumbiji

21 Juni 2013

Shambulio la basi limeripotiwa katika eneo la kati la Msumbiji.Mzee mmoja wa kike amekufa na abiria kumi wamejeruhiwa.Maafisa wa serikali wanawatuhumu waasi wa zamani wa RENAMO kuhusika na shambulio hilo.

https://p.dw.com/p/18tvS
Njia ya reli inaoelekea BeiraPicha: Reuters

Shambulio hilo limejiri siku mbili tu baada ya wafuasi wa RENAMO ambao tangu vilipomalizika vita vya miaka 17 vya wenyewe kwa wenyewe mnamo mwaka 1992 wanajikuta wakikalia viti vya upinzani bungeni,kutishia "kuzuwia" njia zote muhimu za nchi hiyo pamoja pia na njia pekee ya reli inayosafirisha makaa hadi nchi za nje,ili kupata ridhaa za kisiasa kutoka chama tawala cha FRELIMO.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani Perdro Cossa ameliambia shirika la habari la Reuters risasi tatu zimefyetuliwa dhidi ya basi hiyo ya abiria karibu na mji wa Machanga katika mkoa wa Sofala.Habari kutoka ripota wa DW mjini Maputo zinasema bibi mmoja mzee ameuwawa na abria wengine 10 wamejeruhiwa-mmohja hali yake ni mahtuti.

"Sina shaka yoyote upande huo,RENAMO wanahusika na shambulio hilo-amesema msemaji wa wizara ya mambo ya ndani Perdro Cossa.

Hofu za kuzuka machafuko zimeenea

RENAMO-Basis in Inhaminga
Ngome ya RENAMo huko InhamingaPicha: Gerald Henzinger

Kwa mujibu wa shirika la habari la Uingereza Reuters,polisi ya Msumbiji imemkamata mkuu wa kamati ya habari ya chama hicho cha upinzani,JERONIMO MALAGUETA .Msemaji wa RENAMO aliyethibitisha habari hizo amewatolea wito wafuasi wao wakusanyike nje ya jela ya mji mkuu Maputo ambako Malagueta anashikiliwa.

Shambulio hilo pamoja na kumakamatwa Jeronimo Malagueta vinaweza kuzidisha mivutano kati ya chama hicho cha waasi wa zamani na serikali ya Msumbiji inayoongozwa na chama cha FRELIMO.

RENAMO wanakituhumu chama cha FRELIMO kughushi tume ya uchaguzi ili kumhakikishia ushindi mkubwa rais Ernesto Guebuza,uchaguzi wa rais utakapoitishwa mwaka mmoja kutoka sasa.

Wanajeshi wasiopungua 11 na raia watatu wameuwawa kutokana na mashambulio ya tangu mwezi wa April mwaka huu,pale kiongozi wa RENAMO Afonso Dlakama alipotishia kuanzisha wimbi jipya la matumizi ya nguvu ikiwa FRELIMO haitoacha kudhibiti siasa na uchumi wa Msumibiji.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Reuters

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman