Kituo cha Sheria Zanzibar cha laani kukamatwa kwa watu wa Pemba waliowasilisha waraka kwa Umoja wa Mataifa
16 Mei 2008Matangazo
Wananchi hao wakaazi wa Pemba waliwasilisha barua katika Umoja wa mataifa wakitaka kujitenga kwa kisiwa hicho kwa kile walichodai kutopewa umuhimu na serikali ya Zanzibar. Ili kupata ufafanuzi wa Kisheria nimezungumza na Profesa Haroub Othman mwanasheria na mwanaharakati katika kituo cha Sheria na haki za Binadamu Visiwani Zanzibar.