1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kivumbi kikali kati ya Dortmund na Bayern

4 Machi 2016

Vilabu viwili vikuu Ujerumani vitashuka dimbani huku wenyeji Borussia Dortmund wakilenga kuongeza moto katika kinyang'anyiro cha taji la Bundesliga kwa kupunguza hata zaidi pengo kati yao na Bayern Munich

https://p.dw.com/p/1I7QG
Fußball Bundesliga FC Bayern München vs. BVB Borussia Dortmund Tuchel Guardiola
Picha: Imago/Sven Simon[M]

Vijana wa Pep Guardiola walionekana ni kama wanatoroka na kombe lao la nne mfululizo, wakati wakiwa na pengo la pointi nane dhidi ya Dortmund, hadi pale Mainz walipowawekea breki kwa kuwachapa mabao mawili kwa moja Jumatano usiku. Dortmund nayo iliichapa Darmstadt 2-0 na sasa kivumbi cha leo uwanjani Signal Iduna Park kinatarajiwa kuwa cha kusisimua isipokuwa Bayern wanapigiwa upatu. Wakati timu hizo zilikutana mara ya mwisho Oktoba, Bayern iliizaba Dortmund 5-1 mjini Munich.

Kando na kinyang'anyiro cha kutaka ubingwa, kutakuwa pia cha kuepuka kushushwa ngazi wakati Werder Bremen watawaalika washika mkia Hanover. Hoffenheim ambao watasafiri kupambana na Stuttgart. Katika mechi nyingine za leo, Wolfsburg watapambana na nambari nne Borussia Moenchengladbach, VfB Augsburg watapiga dhidi ya Bayer Leverkusen, Eintracht Frankfurt dhidi ya Ingolstadt, Cologne watakuwa nyumbani dhidi ya Schalke. Kesho Jumapili, Mainz watapambana na Mainz v Darmstadt, wakati Hamburg wakipambana na nambari tatu kwenye ligi Hertha Berlin

Mwandishi. Bruce Amani/AFP/AP
Mhariri: Yusuf Saumu