1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Klinsmann amuonya Messi na wenzake

Admin.WagnerD21 Juni 2016

Kocha wa timu ya taifa ya Marekani Juergen Klinsmann ana matumaini kwamba timu yake inaweza kupata ushindi muhimu dhidi ya Argentina katika kombe la Copa America Centenario katika awamu ya nusu fainali

https://p.dw.com/p/1JALi
Copa America 2016 Venezuela vs Argentinien
Picha: Reuters/Winslow Townson-USA TODAY Sports

Wenyeji wa mashindano hayo Marekani watakumbana leo uso kwa uso na kikosi cha Lionel Messi. Kocha wa Marekani Juergen Klinsmann amesema ana furaha kucheza na moja kati ya timu za juu kabisa duniani, Argentina. "Tunafuraha kwasababu tunacheza na moja kati ya timu bora kabisa duniani na hiki ndio mtu anachotaka na hiki ndio unachohitaji kujipima na kujitoa na kupambana nao, nafikiri timu yangu imefanya vizuri sana katika wiki chache zilizopita na kupata zawadi kwa juhudi zao kwa kuingia katika nusu fainali , lakini huu ni wakati ambao hautokei kila wakati katika wakati wako wa kufanyakazi, kwa hiyo kile nitakachowaambia ni kupambana, kuwema na ujasiri na kutambua kuwa mnaweza kufanikiwa, kila timu inaweza kushindwa duniani na kama unaelewa kwamba katika wakati huu hivi sasa tekeleza, jitahidi."

Klinsmann amefikia lengo la kabla ya mashindano hayo la kufikia timu nne za mwisho baada ya kuisaidia timu yake kupita katika kundi lililokuwa na changamoto kubwa katika awamu ya makundi , na robo fainali ambapo iliitoa Ecuador .

Wakati huo huo Argentina inasumbuliwa na ukweli kwamba ilipoteza fainali ya kombe la dunia dhidi ya Ujerumani na pia fainali ya Copa Amerika mwaka jana dhidi ya Chile. Kesho Jumanne Argentina inakumbana na Marekani wakati wakiwania kufa na kupona kunyakua ubingwa huo.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre / ape / afpe / dpae
Mhariri: Yusuf , Saumu