1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Klinsmann kocha mpya wa Bayern Munich

11 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CoQc

BERLIN

Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani Jürgen Klinsmann amechaguliwa kuwa kocha mpya wa timu ya Bayern Munich.

Timu hiyo mashuhuri katika michuano ya ligi kuu ya Ujerumani Bundes Liga imetowa tangazo hilo katika taarifa iliowekwa kwenye tovuti ya mtandao wake.

Klinsmann mwenye umri wa miaka 43 atachukuwa nafasi ya kocha wa hivi sasa wa timu hiyo Ottmar Hitzfeld mwishoni mwa msimu huu wa ligi.

Klinsmann aliifikisha timu ya taifa ya Ujerumani kushika nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Dunia ya mwaka 2006 na aliwahi kuichezea timu hiyo ya Bayern kwa misimu miwili kuanzia mwaka 1995 hadi mwaka 1997.