1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Klopp: Tunajiandaa kwa mapumziko mafupi

21 Mei 2020

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema klabu hiyo inajiandaa kuwa na mapumziko mafupi kati ya misimu kutokana na kutatizwa kwa msimu huu wa kandanda kulikosababishwa na janga la virusi vya corona.

https://p.dw.com/p/3caPa
Jürgen Klopp, Trainer FC Liverpool
Picha: picture-alliance/AP Photo/H. Ammar

Ligi Kuu ya England inatarajia kurudia mechi zake mwezi ujao. Huku kukukiwa kumesalia mechi tisa kwa kila timu msimu kuisha, msimu utakwenda hadi angalau mwezi Julai. Msimu wa 2020-2021 ulikuwa umepangiwa kuanza Agosti 8.

"Leo tumeanza kufanya mazoezi, vyema kabisa, si mazoezi makali ila vijana wangu wanaonekana kuwa katika hali nzuri," alisema Klopp. "hatujui muda kamili tulio nao ila tuna muda wa kujiandaa kuumaliza msimu huu kwasababu sidhani kama kutakuwa na muda mrefu wa mapumziko kati ya msimu huu na msimu ujao," aliongeza kocha huyo wa Liverpool.

Ligi Kuu ya England imeweka Juni 12 kama tarehe ya kuanza kwa mechi ingawa tarehe hiyo inaweza kubadilishwa, na Klopp anasema wachezaji wataanza moja kwa moja kucheza mechi za ligi bila hata kushiriki mechi za kirafiki.