1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kolon. Wawakilishi wa dini walitaka kundi la G8 kupambana na umasikini.

7 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBtw

Wawakilishi wa dini saba duniani wanaohudhuria mkutano mkubwa wa makanisa ya Kiprotestant nchini Ujerumani katika mji wa Kolon, wamewataka viongozi wa kundi la mataifa ya G8 kuchukua hatua madhubuti dhidi ya umasikini duniani.

Azimio lao linaeleza kiwango cha umasikini kuwa ni kashfa na kuwashutumu viongozi wa kundi la G8 kwa kukubali mtindo wa ukuaji wa kiuchumi ambao unapuuzia athari za kijamii.

Mkutano huo wa Kolon umewaleta pamoja watu 100,000, ikiwa ni karibu watu 4,000 kutoka nje ya Ujerumani.

Waumini 26 milioni wa kanisa la Protestant na Waluteri wanawiana kwa idadi na Wakatoliki nchini humo.