1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kombe la Afrika leo

31 Januari 2008

Angola na mahasimu wao Tunisia kila moja yahitaji alao kutoka sare kuingia duru ijayo.Afrika Kusini lazima iishinde Senegal na kutumai Angola au Tunesia inamshinda mwenziwe.

https://p.dw.com/p/D0PJ

DEUTSCHE WELLE 31-01-08

Mapambano 2 yatakuwa uwanjani mjini Kumasi na Tamale jioni hii ili kukamilisha duru ya kwanza ya kombe la 26 la Afrika nchini Ghana:

Tangu Angola hata Tunesia kila moja inahitaji sare au pointi moja kucheza duru ijayo wakati katika mpambano wapili ,Bafana Bafana –Afrika Kusini inanin’giniza matumaini ya mwisho ya kubaki mashindanoni mradi tu imewashinda simba wa terange-Senegal na kutumai Tunesia na Angola –mmojawao anamshinda leo mwenzake.

Angola inahitaji sare kuandika historia ya kucheza kwa mara ya kwanza robo-finali ya kombe la Afrika ambalo Angola itakua mwenyeji wake 2010. Tunesia,mabingwa nyumba ni 2004 ikiongozwa na kocha wao mfaransa Roger Lemerre pia itatosheka na sare wakati Senegal iliopo nafasi ya 3 katika kundi hili ikiwa na pointi 1 tu inaweza ikaokoka endapo itashinda Bafana Bafana-Afrika Kusini na kwa tofauti ya magoli.

Senegal itacheza na kocha mpya-Lamine N’Diaye baada ya kocha wake mpoland Kasperzack kutupa taula ringini akisalim amri baada ya Angola kuikomea mabao 3:1.

Wakati kocha wa Afrika Kusini,mbrazil Carlos Alberto Parreira alisema jana timu yake bado ina matumaini japo madogo ya kuingia duru ijayo,kocha wa Angola Luis Oliveira Goncalves aemearifu kwamba Angola leo hailengi shabaha ya kutoka sare,bali itacheza kushinda.Angola na tunisia kila moja ina pointi 4 kutoka mechi 2 za kundi D wakati Senegal na Afrika Kusini zinazocheza wakati mmoja huko Kumasi kila moja ina pointi 1.

Senegal imetangaza marufuku ya kutoa habari kutoka kam bi yake.Kisa nini ? Hii imefuatia kuchapishwa habari katika magazeti ya Ghana kuwa nahodha wao El hadj Diouf alikuwa nje hadi usiku wa manane tena masaa 48 kabla ya mpambano huu na Afrika kusini.

Nje ya changamoto za leo,nahodha wa Ghana Michael Essien , hatahudhuria sherehe ya kesho mjini Lome,Togo-jirani na Ghana ya kumtunza „mwanasoka bora wa mwaka wa Afrika.“Hii imetangazwa na kocha wake Claude Leroy.Stadi huyo wa chelsea ni miongoni mwa majina yaliopo kwenye orodha fupi ya CAF ya wachezaji bora wa mwaka.

Fredderic Kanoute wa Mali,ambae timu yake imeshapigwa kumbo nje ya kombe hili la afrika ameruhusiwa kwenda Lome kwa sherehe ya kesho.Kanoute stadi wa klabu ya Sevilla ya Spian, ni mmoja kati ya mastadi hao wanaoweza kuvaa taji hilo pamoja na didier Drogba na Michael Essien.

Kabla sherehe hiyo,nahodha wa corte d’Iviore Drogba anaeichezea Chelsea ya uingereza kama essien,amedai klabu za Ulaya zina mapendeleo dhidi ya wachezaji wa kiafrika.

Drogba ameuambia mtandao wa wafadhili wa dimba mtn.football .Com kuwa anaamini kwa dhati kwamba ukiwa ni mchezaji wa kiafrika hutendewi sawa.Binafsi,Drogba amesema amekuwa mateka wa desturi hiyo ya kuwahini wachezaji wa kiafrika kimalipo.Huambiwa ukitaka chukua ,hutaki basi.