1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kombe la Ulaya la Matifa

Ramadhan Ali28 Machi 2007

Kinyan'ganyiro cha kuania tiketi za finali ya Kombe la Ulaya kinaendelea leo kwa Uingereza kucheza na andorra na Itali na Scotland miongoni mwa mapambano kadhaa.Ujerumani ina miadi na Denmark katika dimba la kirafiki.

https://p.dw.com/p/CHcR

Kinyan’ganyiro cha kuania tiketi za kombe la Ulaya la mataifa 2008 nchini uswisi,kinarudi uwanjani jioni hii kwa mabingwa wa dunia-Itali wakiwa na miadi na Scotland wakati Uingereza inakutana na chipukizi Andorra.

Ujerumani ilioitimua majuzi Jamhuri ya Czech kwa mabao 2:1 mjini Prague,iko nyumbani leo kwa mpambano wa kirafiki na Denmark mjini Duisburg.

Kocha wa Itali Roberto Donadoni ana kibarua kigumu katika zahama ya leo na waskochi kama alicho nacho wakati huu kocha wa Uingereza Steve McClaren.Kwani,Uingereza inahitaji kuziba mwanya na kuondoka bila ya taabu na pointi 3 leo kwa kuipiga kumbo Andorra ama sivyo,maji kwake yatazidi unga.

Donadoni anabidi kuipiku Scotland inayoongoza kundi lao baada ya waskochi kuwatimua Georgia 2-1.Jamhuri ya Czech ilioakndikw amabao 2:1 na Ujerumani jumamosi iliopita inacheza na Cyprus.

Kuna changamoto nyengine nje ya kombe la ulaya:Ecuador yacheza na Mexico,marekani na Guatamala.

Ujerumani inaikaribisha Denmark nyumbani mjini Duisburg.

Kocha wa Ujerumani,Joachin Loew,ameamua kuteremsha takriban timu mpya kwa mpambano wa leo.Akimuacha nje nahodha Michael ballack na kipa Jens Lehmann.Usoni tena ataongoza mashambulio Kevin Kuranyi alieachwa nje ya Kombe la dunia mwaka jana.

Jana kulikuwapo pia na changamoto kadhaa za kirafiki za timu za Taifa.Ghana au Black Stars ilikutana tena na Brazil tangu mkutano wao katika Kombe la dunia hapa Ujerumani.Mara hii Brazil iliondoka na ushindi wa bao 1:0 huko Sweden.

Mara hii jana, Dunga kocha wa Brazil alietumia washambulizi 3 :Ronaldinho,Kaka na Robinho kuitandika Chile mabao 4:0 mwishoni mwa wiki,aliamua kuimarisha ngomed zaidi dhidi ya Black Stars.Love anaeichezea CSKA Moscow ndie alieufumania mlango wa Ghana kwa bao pekee hiyo jana.

Real Madrid ya Spian inapanga kujaribu kuwasajili msimu ujao Cristiano Ronaldo kutoka Manchester United na Kaka kutoka AC Milan kujiunga nayo.

Real pia inapigiwa upatu kuwa inataka kumuajiri mlinzi wa Borussia Dortmund ya Ujerumani, Christoph Metzelder anaetarajiwa kuiaga Dortmund mwishoni mwa msimu huu.

Medali 2 za dhahabu zimeenda afrika katika mashindano ya ubingwa wa dunia ya kuogolea huko Melbourne,Australia:Oussama Mellouli amekuwa mtunisia wa kwanza kuibuka bingwa wa dunia katika hodhi la kuogolea alipowasangaza mahasimu na kushinda leo mita 800 mtindo huru-freestyle.

Mellouli mwenye umri wa miaka 23 alitia for a masafa ya mita 100 ya mwisho na kushinda kwa muda wake wa dakika 7:46.95.

Tunisia ni maarufu katika dimba barani Afrika na sasa imeandika historia katika hodhi la dunia la kuogolea.

Medali nyengine ilioenda Afrika leo, ilinyakuliwa na Muafrika Kusini, Cameron van der Burgh.Yeye alilenga katika finali ya mita 50 “backstroke” kutomaliza wa mwisho na alipomaliza wa tatu na kwa medali ya shaba, hakuamini macho yake.

Katika orodha ya dunia huko Melbourne, Russia inaongoza kileleni ikifuatwa na China huku Marekani ikisimama nafasi ya 3.Tunisia inafuata nafasi ya 7 nyuma ya Ujerumani.