1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Korea Kusini yakubali majeshi yake kubaki Iraq huku 10 wauawa na bomu Baghdad

28 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/ChZD

SEOL:

Bunge la Korea kusini limepiga kura na kuunga mkono kurefushwa kwa mda wa vikosi vyake wa kubaki nchini Iraq.

Vikosi hivyo vilitumwa huko mwaka mmoja uliopita.Wabunge wengi wameunga mkono kurefushwa kwa mda huo hadi Disemba mwaka wa 2008.Hata hivyo idadi yao wanasema lazima ipunguzwe kufikia wanajeshi 650.

Korea Kusini ilituma askari 3,600 nchini Iraq mwaka wa 2004,lakini idadi yao imekua ikipungua kutokana na shinikizo la wananchi nchini Korea wanaopinga kupelekwa huko.Kwa sasa wanajeshi wa Korea kusini walioko Iraq wanafikia 1,200na wako katika eneo lililo salama la wa Kurdi.

Kwa mda huohuo taarifa kutoka Iraq zasema kuwa watu wasiopungua 10 wameuawa na wengi zaidi kujeruhiwa kufuatia bomu lililo lipuka katika soko mjini Baghdad. Soko ambalo ni marufu, lilikuwa limejazana watu waliokuwa wanaelekea nyumbani baada ya sala ya ijumaa wakati wa bomu lilipotokea.Polisi imesema wahanga wote walikuwa raia wa kawaida.