1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mpango wa kutaka kumuuwa Kim Jong kwa silaha za biokemikali

12 Mei 2017

Korea ya Kaskazini imeagiza kuondolewa kwa mkuu wa upelelezi wa Korea ya Kusini kwa madai kuwa alikuwa na mbinu za kumuuwa kiongozi wa Korea ya kaskazini, Kim Jong Un, kwa kutumia silaha za biokemikali,

https://p.dw.com/p/2crD9
Nordkorea Kim Jong-un
Picha: Reuters/KCNA

 Huku shirika la habari la nchi hiyo, KCNA, limelituhumu shirika la ujasusi la Marekani na Korea ya Kusini kuwa na mpango wa kutaka kumuua kiongozi wao mtakatifu kwa kutumia silaha za biokemikali.

Kauli hiyo imekuja baada ya wiki mbili za kauli kutoka Marekani, China na Korea ya Kusini  juu ya maendeleo ya silaha za nyuklia na makombora ya Korea ya Kaskazini pamoja na kuwepo kwa hofu juu ya Korea Kaskazini kufanya jaribio lake la sita ya makombora, ikipuuzilia mbali maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Hapo jana, Korea ya Kaskazini ilidai ikabidhiwe "mtuhumiwa wa ugaidi" anayehusika na mpango huo wa kutaka kumuuwa kiongozi wake, Kim Jung-Un, ingawa mpaka sasa haijasema mtuhumiwa huyo ni nani.

Ofisi ya Mwendesha Mashitaka imesema hivi leo (Ijumaa 12 Mei) kupitia kituo cha habari cha KCNA kuwa kiongozi mkuu wa mpango wa mauaji hayo ni Mkuu wa Shirika la Ujasusi la Korea ya Kusini Lee Byung-ho, na wachunguzi wengine wawili wa Korea ya Kusini na Mchina mmoja.

"Tunazitaka mamlaka husika ziwatafute, ziwakamate na kuwakabidhi washutumiwa hao kwa DPRK haraka iwezekanavyo," ilisema ofisi ya kuendesha mashtaka .

Washutumiwa hao wanakabilio na adhabu kali endepo watakamatwa kwa sababu sheria ya korea ya kusini ya uhalifu huwa ina adhabu kali sana.

Lee alikuwa mkuu wa shirila la ujasui la Korea ya Kusini la NIS chini ya utawala  awali wa kihafidhina wa Korea ya Kusini. rais mpya wa Korea ya Kusini amemteuwa mtu mpya kushikilia nafasi hiyo, lakini bado Lee anaendelea kuwepo ofisini mpaka mteuliwa huyo akubalike.

Shirika la upelelezi la Korea ya kusini NIS limesema mapema kuwa hutuma hizo za Korea ya Kusini hazina uthibitisho wowote. NIS ilisema Ijumaaa kuwa haina habari yoyote juu ya shutuma za Korea ya kaskazini na Lee hakuwa na lolote la kusema.

Shirikala la upelelezi la Marekani na Ikulu ya Marekani imekataa kutoa kauli yoyote juu ya kauli ya Waziri wa usalama wa serikali wa Korea ya kaskazini iliyotelewa wiki iliyopita.

Korea ya kaskazini ilisema kuwa wasimamizi wa usalama wa Marekani na Korea ya Kusini ilipanga kumshambulia Kim Jong Un kwa silaha za biokemikali tarehe 15 Aprili katika sherehe za kusheherekea kuundwa kwa taifa hilo na Kim II Sung.

Mjumbe wa Korea ya Kaskazini katika Umoja wa Mataifa alisema Alhamis kuwa mpango wa kutaka kumuuwa kiongozi wao ni tamko la vita.

Mwandishi: Najma Said/AFPE

Mhariri: Mohammed Khelef