1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kufukuzwa kwa wafanyakazi haramu Saudi Arabia kwazorotesha huduma za jamii

Admin.WagnerD14 Novemba 2013

Mpango wa kuandamwa kwa wahamiaji haramu Nchini Saudi Arabia umesababisha maduka kufungwa na hofu miongoni mwa wananchi, huku huduma za jamii zikiwa zimepungua kufuatia kukosekana kwa wafanyakazi.

https://p.dw.com/p/1AHQ1
Mfalme wa Saudi Arabia, Al-Faisal bin Abdulaziz al-Saud akiwa na Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry.
Mfalme wa Saudi Arabia, Al-Faisal bin Abdulaziz al-Saud akiwa na Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry.Picha: Reuters

Taka zimezagaa mitaani, hadi kwenye maeneo yanayozunguka misikiti, na viwanda kadhaa vimefungwa. Hofu ni kubwa miongoni mwa wageni hao na wenyeji wao, na sasa athari za kiuchumi na kijamii za operesheni hiyo ya Saudi Arabia dhidi ya wafanyakazi wa kigeni ziko wazi.

Wafanyakazi wengi wa kigeni ndio waliokuwa wakifanya kazi hizo ndogo ndogo zenye pato la chini, ambazo wenyeji huwa hawazigusi. Sasa huduma nyingi zimesitishwa ikiwemo kufungwa kwa maduka ambapo pia nusu ya kampuni za za ujenzi zimelazimika kusimamisha huduma zake.

Haya yanakuja katika wakati ambapo Saudi Arabia inatekeleza agizo lake la kuwaondosha kwa nguvu wafanyakazi wa kigeni wapatao milioni 9 walioko huko kinyume na sheria. Operesheni hiyo iliyoanza tangu wiki moja na nusu iliyopita imekuwa ikiendeshwa kibabe na hivyo kupelekea vurugu na hata mauaji.

Kumiminika kwa wageni nchini Saudi Arabia kumesababishwa na wenyeji kukataa kufanya kazi zenye kipato kidogo na hivyo kuwaachia wageni wanaoridhika na kiwango hicho cha chini cha mshahara, ingawa kwa mujibu wa Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF, kiwango cha ukosefu wa ajira miongoni mwa wazawa kimeongezeka kufikia asilimia 12.1 mwaka jana.

Jambo ambalo limeifanya serikali ya Saudi Arabia kutoa onyo kuhusu kuongezeka kwa wageni, ambapo mamia ya wafanyakazi wa kigeni wamekuwa wakirudishwa baada ya kuingia nchini humo kwa njia zisizohalali huku wengine wakifanikiwa kupata hati ya kuendelea kuishi kupitia mpango wa msahamaha wa mfalme.

Shule 20,000 zakosa wafanyakazi

Wakati mpango huo ukimalizika umemalizika wiki iliyopita , watu 33,000 wamenufaika huku wengine wakiendelea kujificha, na hivyo sekta nyingi kubaki na wafanyakazi wachache ambapo inaripotiwa kuwa shule 20,000 elfu hivi sasa zimebaki bila waangalizi huku nyingine zikikabiliwa na changamoto ya kukosa usafiri wa wanafunzi.

Wahamiaji wa kigeni hufanya kazi zenye kipato cha chini.
Wahamiaji wa kigeni hufanya kazi zenye kipato cha chini.Picha: Abdelhak Senna/AFP/GettyImages

Kwa mujibu wa rais wa jumuiya ya biashara na uchumi ya kimataifa, Khalaf al-Otaibi, asilimia 40 ya kampuni ndogo ndogo za ujenzi zmesimamisha huduma zake kutokana na wafanyakazi wake wengi kukosa hati halali za kuishi.

Hata hivyo, kwa mujibu wa mtafiti wa haki za binaadamu mashariki ya kati, Adam Coogle, ikiwa Saudi Arabia itataka kufanya kazi hiyo kwa umakini, inapaswa kuangalia zaidi upande wa sheria lakini kwa kuwalenga wafanyakazi moja kwa moja.

Kwa upande wake mmiliki wa kampuni moja kubwa mjini Riyadh, ambaye hakutaka kutaja jina lake, ameliambia shirika la habari la IPS kuwa amelazimika kufunga miradi mingi kwa kukosa wafanyakazi, na kwamba si suala la busara kuwafukuza wafanyakazi ambao wamekuwa wakifanya kazi kwa miaka sasa.

Amesema haiwezekani kuwafukuza watu namna hiyo wakati wamefanyakazi kwa muda mrefu sasa.

Raia wa Sudan auawa katika vurugu

Mwishoni mwa wiki iliyopira, wakazi wa eneo la Manhoufa mjini Riyadh walizusha vurugu baina ya raia wa Ethiopia na wengine kushikiliwa hadi hapo Jeshi la polisi lilipowasili katika eneo la tukio zaidi ya masaa mawili baada ya tukio.

Saudi Arabia katika shughuli za kijamii
Saudi Arabia katika shughuli za kijamiiPicha: picture-alliance/Landov

Ghasia hizo zliibuka tena katika eneo hilo na kusababisha kifo cha raia mmoja wa Sudan kupoteza maisha.

Mwandishi: Flora Nzema/APE

Mhariri: Mohamed Khelef