1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

"Kundi la Mashauriano kuhusu Libya" lakutana Abu Dhabi

9 Juni 2011

Zaidi ya mawaziri 20 wa mambo ya nchi za nje na wawakilishi kutoka mashirika ya kimataifa wanajumuika leo (09.06.2011) huko Abu Dhabi, kwa mkutano wa tatu wa kundi la mashauriano kuhusu Libya.

https://p.dw.com/p/11XUY
Waasi nchini LibyaPicha: dapd

Mkutano huo utaongozwa na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Umoja wa flame za kiarabu Sheikh Abdullah Bin Zayed Al-Nahyan pamoja na waziri mwenzake wa Italia Franco Frattini.

Hillary Clinton
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary ClintonPicha: AP

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa marekani Hillary Clinton pia aliwasili Abu Dhabi jana kuhudhuria mkutano huo. Aidha taariafa kutoka Brussels kwenye makao makuu ya Jumuiya ya kujihami ya NATO zimesema wawakilishi wa jumuiya hiyo pia wanahudhuria mazungumzo hayo, sambamba na wale kutoka Umoja wa Afrika, Umoja wa mataifa, Umoja wa Ulaya na Umoja wa nchi za kiarabu.

Kwa upande mwengine Ujerumani ambayo ilikataa kushiriki katika kampeni ya mashambulizi ya anga dhidi ya ngombe za utawala wa Gaddafi, imesema pamoja na hayo iko tayari kusaidia ujenzi mpya wa nchi hiyo mapigano yatakapomalizika. Akizungumzia utayarifu huo,

Mkutano huo wa kundi la mashauriano kuhusu Libya utazungumzia hatua zinazohitahjika ili kuimarisha utaratibu wa msaada wa fedha kwa baraza la taifa la mpito nchini Libya linaloongozwa na wanaoupinga utawala wa Gadadafi na ambalo makao yake makuu yako katika mji wa mashariki wa Benghazi.

Utaratibu maalum wa kulisaidia kifedha ulianzishwa wakati wa mkutano wa pili wa kundi hilo, uliofanyika Roma, Italia mwezi uliopita. Mkutano wa kwanza mwezi Aprili katika taifa la Ghuba la Qatar ulimtaka Gaddafi aondoke madarakani, jambo ambalo kiongozi huyo hadi sasa analikaidi.

Gaddafi mwenye umri wa miaka 69 aliuambia umoja wa Afrika hivi karibuni kwamba atakubali usimamishaji mapigano na waasi, lakini hayuko tayari kun´goka madarakani. Maelfu ya raia wanahofiawa wameuawa tangu mgogoro wa Libya ulipoanza mwezi Februari.

Wakati huo huo, mashambulizi ya NATO yameendelea dhidi ya mji mkuu Tripoli. Jana jioni miripuko mikubwa ilisikika karibu na makaazi ya kiongozi wa Libya mjini humo.

Naye rais Abdoulaye Wade wa Senegal ambaye amelitambua baraza la mpito la taifa nchini Libya kuwa muwakilishi halali wa ummoa wa nchi hiyo anatazamiwa kuwasili Benghazi leo kwa mazungumzo na viongozi wa baraza hilo, wakati shinikizo la kumtaka Gaddafi aondoke madarakani likiongezeka.

Mwandishi: M. Abdul-rahman

Mhariri: Oummilkheir Hamidou