1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kundi la mataifa manne yenye usemi zaidi katika mzozo wa mashariki ya kati linasema hali ya Gaza si nzuri

Kalyango Siraj2 Mei 2008

Pia limetaka kukomeshwa kwa uvurumishwaji wa maroketi kwa Israel

https://p.dw.com/p/DsUC
Kutoka kushoto, waziri mkuu wa Uingereza, Gordon Brown, waziri mkuu wa Mamlaka ya Palestinian Salam Fayyad na waziri mkuu wa zamni wa Uingereza r Tony Blair, wakishiriki katika mkutano kuhusu Palestinian mjini London, Alhamisi, May 1, 2008. Baadhi ya mataifa ya kiarabu yamelaumiwa kwa kutotimiza ahadi ya kusaidia mamlaka hiyo kwa hali na mali.Picha: AP

Kundi lenye usemi zaidi katika mzozo wa Mashariki ya Kati, linaloweza kuitwa la washika dau wakuu wanne wa Mashariki ya Kati,limeitaka Israel na mamlaka ya Palestina kuheshimu ahadi za kuendeleza mazunguzo ya amani.

Kwa mda huohuo mataifa ya kiarabu yamekosolewa na utawala wa Marekani kwa kushindwa kutimiza ahadi za kifedha kusaidi mamlaka ya Palestina,kuendesha shughuli zake.

Hayo ni baadhi ya matokeo ya mkutano kuhusu Mashariki ya kati uliofanyika mjini London nchini Uingereza.

Kundi hilo lenye ushawishi mkubwa katika mzozo wa mashariki ya kati linawajumulisha washika dau wanne.

Washika dau hao ni Marekani,Urusi,Umoja wa Ulaya pamoja na Umoja wa Mataifa.Na katika lugha geni wanaitwa,The Middle East Quartet.

Na kiongozi wake ni waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair.

Katika mkutano uliofanyika London,kundi hilo miongoni mwa mengine limesikitishwa na hali ilivyo katika ukanda wa Gaza.Katika taarifa ya pamoja baada ya mkutano huo iliosomwa na katibu mkuu wa Umoja wa mataifa, Ban Ki-moon,kundi hilo pia limeonesha kutofurahishwa kwao na hatua kadhaa za Israel kuhusu makazi.

Kundi hilo limeomba kuendeleza msaada sio tu wa dharura lakini pia wa kibinadamu katika eneo la Gaza bila kizuizi. Hali ya sasa katika eneo hilo imeelezwa na Tony Blair kama ya kusikitisha.

kabla ya mkutano wa London, mashirika ya kimisaada, kama vile shirika la Oxfam, yalikuwa yamelihimiza kundi hilo kuutumia mkutano huo kuishinikiza Israel kuondoa vikwazo ilioviwekea eneo la Gaza.

Shirika hilo limeonya kuwa janga la kibinadamu linanukia Gaza kutokana na vikwazo hivyo ambavyo vinayafanya maisha ya watu wa kawaida kuwa magumu mno,kwani imeyawia vigumu mashirika ya kutoa msaada kufanya kazi.

Yeye waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier ametoa ushauri kwa watu wote wa eneo la Mashariki ya Kati.

Kuhusu mataifa mengine ya kiarabu kundi hilo limewahimiaza wahisani kutimiza ahadi za kisiasa na kifedha yalizotoa kusaidia watu wa Palestina katika mkutano wa Paris wa Disemba 2007.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani Bi Condoleezza Rice,ambae almepitia london katika safari yake ya mashariki ya Kati ameyalaumu mataifa ya Kiarabu ambayo yameshindwa kutekeleza ahadi yalizotoa kusaidia malaka ya Palestina.

Maafisa wa Marekani wanasema kuwa ni takriban ya asili mia 20 tu ya fedha ambayo imelipwa na mataifa yote ya kiarabu yalitoa ahadi.

Ingawa Rice hakutaja mataifa hayo yaliyoshindwa kutekeleza ahadi lakini afisa mmoja wa Marekani,amesema kuwa serikali yake inamatumaini kuwa pesa zaidi zitapatikana,akiongeza kuwa ni Saudi Arabia,Umoja wa falme za Kiarabu na Algeria tu ndizo zimelipa ada zake za mwaka huu zinazofikia dola za kimarekani millioni zaidi ya 153.

Idadi ilioahidiwa ni takriban zaidi ya dola billion 1 kwa bajeti ya mwaka huu wa 2008.

Wahisani wengine wa nchi za magharibi wamechangia dola millioni 500 na Ushei.Wahisani hao ni Marekani,Umoja wa Ualya,Uingereza,Norway na Ufaransa.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani amesema kuwa lingekuwa jambo zuri ikiwa ahadi zinatimizwa.

Afisa mmoja wa Marekani amezitaja nchi za kirabu ambazo hazijatoa mchango wake vile Kuwait,na Qatar.