1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kunguru wazusha tafrani Canada

Sudi Mnette
29 Juni 2017

Shirika la huduma za kusafirisha vifurushi mjini Vancouver, Canada limesitisha huduma zake kutoka na vitendo vya uvamizi na uporaji vinavyofanywa na kunguru nchini humo.

https://p.dw.com/p/2febM
Eine Gruppe von Raben
Picha: picture alliance/blickwinkel/D. & M. Sheldon

Kwa wale wenye umri wa wastani wanaweza kukumbuka katika jiji la Dar es Salaam na maeneo ya karibu hasa ya mkoa wa Pwani watakumbuka uporaji ule uliokuwa ukifanywa na kunguru mpaka jiji likianzaisha mpango maalumu ya kuwaangamiza kungura hao. Waliuwawa kwa bunduki na maeneo mengine kulitumika mitego ya aina fulani. Walikuwa wanafanya mengi lakini miongoni mwa hayo ilikuwa wanaweza hata kupora kofia kwa wakazi walikuwa ndani ya kivuko kuelekea Kigamboni. Sasa jambo kama hilo limejirudia lakini safari hii limetokea Vancouver Canada.

Si jambo la mzaa, mpaka Shirika la Posta lenye dhamana ya kusambaza vifurushi limesimamisha jukumu hilo. Kwa taarifa yake shirika hilo limesema uamuzi huo unatakona ana mashambulizi ya mara kwa mara ya kunguru. Kwa mujibu wa shirika la habari la Ufaransa AFP hivi karibuni kunguru hao walifanya mashumbulizi kwa mbeba vifurushi ambae alikuwa akiwasilisha barua hizo katika nyumba tatu toafuti ambapo pamoja na kunyakua kifurushi alikwaruzwa vibaya. Kutokana na hali kuwa mbaya ya uvamizi wa aina hiyo ya kunguru wakazi katika vitongoji vya jiji la Vancouver wameelekezwa pa kupeleka baura zao.

Mwandishi: Sudi Mnette
Mhariri: Mohamed Khelef