1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kupambana na wimbi la wahamiaji - Uhamiaji mijini

1 Juni 2011

Wakati ambapo idadi ya ikipungua maeneo ya vijijini, barani Afrika, miji mikubwa imeshuhudia ongezeko kubwa la maeneo ya mabanda.Wahusika wakuu katika mchezo wetu wa radio wanavunja tabia hiyo na kureja vijijini kwao

https://p.dw.com/p/OzRC
Picha: LAIF

Wengi wanajaribu bahati yao katika miji mikubwa baada ya kuona kwamba hakuna nafasi ya maisha kwenye maeneo yao ya vijijini.Lakini si rahisi hivyo, kuweza kufanikiwa katika miji iliyofurika watu barani Afrika.Wengi wa wahamiaji wanapowasili katika miji hiyo hugundua kuwa si sehemu waliyokuwa wakiidhania ingeweza kutimiza ndoto zao za kuwa na kazi na maisha mazuri.

Katika mfululizo wa vipindi vyetu vya Learning by Ear, Ben na rafiki zake Baki na Zeina wameamua kupambana dhidi ya fikra fulani.Wakitishwa na kiza kilichoko mjini juu ya mustakhbali wa maisha yao, vijana hawa watatu waliyohitimu chuo kikuu wanaanzisha chama cha ushirika cha kilimo kijijini kwao.

Changamoto nyingi zinawasubiri na kuingia katika mtihani mgumu.Wapi watapata fedha za kuanzishia mradi wao huo?Je wanakijiji wataupokea vipi mradi huo? Na ni aina gani ya zao ambalo linafaa kwa manufaa ya baadaye na wakati huo huo kuwa na faida? Sikiliza kwa makini kujua iwapo Ben na rafiki zake watafanikiwa!

Kipindi cha Learning by Ear kinapatikana katika lugha sita: Kiingereza, Kiswahili,Kifaransa, Kihausa, Kireno na Kiamaric. Kinafadhiliwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani.