1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kura ya maoni juu ya katiba ya Misri

28 Machi 2007

27% ya wapigakura wmeidhinisha makgeuzi 34 ya katiba ya Misri.wakati serikali yatafsiri huo ni ushindi wengine wanadai ni ushindi wenye dosari.wapiga kura wengi hawakupiga kura zao.

https://p.dw.com/p/CHHK

Misri imepiga kura ya maoni yenye dosari juu ya katiba:Kwa jicho la serikali lakini, mageuzi makubwa ya katiba yameidhinishwa kwa wingi mkubwa na wananchi.Huo kwahivyo, ni ushindi wazi kwa rais Hosni Mubarak-lakini, wenye dosari.

Waziri wa nje wa Marekani Dr.Condoleeza Rice, hakupata marafiki wakati wa ziara yake ya hivi punde nchini Misri.Kabla kuwasili kwake huko alisifu Misri kwa mchango wake muhimu katika mzozo wa Mashariki ya kati.Akaongeza lakini, amestaajabishwa kuiona Misri, haikufungua bado mlango wa demokrasia ya kweli ya vyama vingi ambayo imeanza kutambaa katika Mashariki ya kati.

Mjini Cairo, iliwasangaza viongozi,kwani wakihisi ni mkondo huo hasa, ndio wanaoufuata.Kwani, wakati huu mageuzi hadi 34 yamefanyiwa katiba ya Misri.Wajumbe wa serikali ya Misri wamejikuta lakini peke yao walio na maoni kama hayo.Kwani hata kwa muujibu wa tarakimu rasmi za serikali ya misri walioshiriki katika kura ya maoni juu ya mageuzi ya katiba ni 27% tu ya wapiga kura wakati upinzani unadai hata hao hawakutimia ni chini kabisa ya kima hicho .

Kwamba kura hiyo ya maoni ingepata wingi hakujakuwa na shaka kama ilivyo desturi ya chaguzi zinazofanywa nchini Misri.

Siku zijazo hali itabainika wazi zaidi unadai upinzani na hata wachunguzi.Kwani siku zinazokuja, hakuna chama wala mtetezi atakaeruhusiwa kugombnea uchaguzi nchini Misri akiwakilisha jukwaa la kidini.

Hii ni hatua kwakweli, inayolengwa dhidi ya chama kilichopigwa marufuku lakini kilifumbiwa macho kushiriki katika uchaguzi uliopita-chama cha ndugu wa kiislamu-Muslim brotherhood-chama chenye wafuasi wengi miongoni mwa raia wa kawaida.

Rasmi, inatafsiriwa hatua hiyo, kuwa ni kukandamiza ugaidi.Lakini, inaulizwa kwanini mahakimu hawakuruhusiwa kusimamia kura hii ya maoni ?

Hapo upinzani unaona kuwa serikali ya misri inataka kuidhinisha matokeo ya uchaguzi kama ilivyokua desturi hapo zamani bila vyombo vya kisheria.

Rais mkongwe Hosni Mubarak, ameruhusu kuchomolewa nadharia nyingi za ujamaa katika katiba na kuingiza badala yake “demokrasia ya ubinafsi” lakini mageuzi hayo,hayajumlishi yale yanayohitajiwa na Jamhuri hii ya Misri ambayo wengi waliyatazamia.

Kwa hali ya sasa,mtetezi wa urais aweza tu kuteuliwa na chama kimoja tu ambacho kina alao 3% ya wabunge bungeni.Na hii inamfungulia wazi mlango mtoto wa rais Hosni Mubarak-Gamal -kurithi wadhifa wa baba yake.

Yule asieridhika na hayo anayakosoa mageuzi hayo ya katiba kwavile yanampa kabisa rais mamlaka ya kupiga vita ugaidi.Wakosoaji wanadai ile hali ya hatari iliokuwapo tangu kuuwawa kwa Anwsar Sadat sasa inaingizwa katika katiba.

Katika kambi ya magharibi, hakuna sauti ya kuikosoa katiba hiyo iliosikika hadi sasa.

Kwani, utulivu unaonekana ni bora kuliko demokrasia.Hata ikiwa utulivu huo, umejengewa ukuta wa magereza .Ndio maana matamshi ya waziri wa nje wa Marekani dr.Rice hayaendi sambamba na na unavyofikiri uongozi nchini Misri.Lakini, huko Cairo hakuna atakejali alioyasema.

Kwani, tangu mawaziri wa nje wa Marekani hata marais, huenda huko Cairo na kuondoka .Mjini Cairo lakini,hakuna mabadiliko-uongozi ni ule ule na zimechukuliwa hatua kubakisha hali hiyo.