1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kura ya maoni nchini Zanzibar yapigwa leo.

31 Julai 2010

Wapiga kura laki nne wanatarajiwa kushiriki katika kura ya maoni.

https://p.dw.com/p/OYwj
Kisiwa cha Zanzibar kilijitangazia uhuru wake tarehe 12 Januari 1964.Picha: picture alliance/dpa

Kura ya maoni nchini Zanzibar inapigwa leo yenye lengo la kuamua ikiwa itakuwa na serikali ya umoja wa kitaifa baada ya uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba ili kusitisha uhasama uliokita mizizi na kuvuruga maendeleo katika kisiwa hicho cha Tanzania kwa miongo kadhaa.

Afisa mkuu wa polisi katika mji mkuu wa Zanzibar, Stone Town, Aziz Juma amedhihirisha kwamba uchaguzi unaendelea vizuri na kwamba wanatarajia utakuwa wa amani.

Sansibar Stonetown
Mji mkuu, Stone Town. Zanzibar ina idadi ya raia milioni 1.2.Picha: DW /Maya Dreyer

Wapiga kura laki nne wanatarajiwa kushiriki katika Uchaguzi huo unaonuia kupitisha pendekezo la kufanywa marekebisho katika katiba yatakayotenga nyadhifa mbili za makamu wa rais zitakazogawanywa kati ya vyama vitakavyoshika nafasi ya kwanza na ya pili katika uchaguzi wa wawakilishi.

Zanzibar ilijitangazia uhuru wake tarehe 12 Januari mwaka wa 1964 baada ya mapinduzi ya umwagaji damu uliokamilisha karne kadhaa za utawala wa Masultani wa Kiarabu.

Uhasama kati ya chama kikuu cha CCM na CUF katika kisiwa hicho cha watu milioni 1.2, umekuwa ukikithiri na wakati mwingine kusababisha umwagaji damu tangu kuanzishwa kwa sera ya vyama vingi mwaka wa 1992.