1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kura ya maoni yapigwa Zanzibar na Pemba

31 Julai 2010

Wananchi visiwani Unguja na Pemba leo wanapiga kura ya maoni kuamua iwapo kuundwe serikali ya umoja wa kitaifa ili kumaliza migogoro ya mara kwa mara kuhusu uchaguzi visiwani humo.

https://p.dw.com/p/OYlU
Ras Nungwi village is famous for wonderful beaches and for his shipyards, Insel Zanzibar, Tansania
Pwani maarufu ya kijiji cha Ras Nungwi kisiwani Zanzibar.Picha: picture-alliance / Bildagentur Huber

Chama tawala cha CCM na chama kikuu cha upinzani cha CUF, vinaunga mkono kura hiyo ya maoni na vimetoa mwito kwa wananchi kuipigia kura ya "ndio."

Kuambatana na muundo mpya wa serikali hiyo, Zanzibar itakuwa na rais alie na makamu wawili. Makamu wa kwanza wa rais atatoka katika chama kitakachoshika nafasi ya pili katika uchaguzi na makamu wa pili atatokea chama kitakachoshinda.Mawaziri watachaguliwa kwa kuzingatia misingi ya uwiano.

Iwapo kura hiyo itapitishwa,katiba ya Zanzibar itafanyiwa marekebisho, ili kufungua njia ya kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa kwa matayarisho ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanywa Oktoba 31 mwaka huu wa 2010.