1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kurejeshwa kwa wapiganaji wa FDLR Rwanda

1 Agosti 2008

Nchini Kongo wapiganaji 67 wa kundi la waasi la FDLR wamejisalimisha kwenye kambi ya Masiki eneo la Mashariki.Shughuli hiyo ilifanyika hapo jana mkoani Kivu ya Kaskazini.

https://p.dw.com/p/EoeB
Mwanajeshi wa Umoja wa Mataifa nchini KongoPicha: AP

Ujumbe wa Umoja wa mataifa nchini Kongo MONUC ulio mkubwa zaidi ulimwenguni umekuwa ukihusika na shughuli ya kuwarejesha kwao Rwanda wapiganaji hao wa FDLR.Itakumbukwa kuwa mwaka 2005 kundi hilo la FDLR lilitangaza kuwa linataka kurejea nyumbani kwao Rwanda vilevile kusitisha mapigano.Tamko hilo lilitolewa mjini Roma nchini Italia chini ya upatanishi wa jamii ya Sant'Egidio.

John Kanyunyu alihudhuria shughuli hiyo na kututumia taarifa ifuatayo.