Iddi Mohammed Mwimbe kutoka Bagamoyo, Tanzania, ana umri wa miaka 28 tu lakini tayari ameshachapisha diwani mbili za ushairi kwa nguvu zake mwenyewe, na hivi karibuni alikuwa mshindi wa Tuzo ya Ibrahim Hussein ambayo inawashajiisha washairi chipukizi nchini humo. Hapa anazungumza na Mohammed Khelef juu ya safari yake ya ushairi.