1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kutekwanyara wajerumani 3

14 Julai 2008

Juhudi zaendelea kuwakomboa wajerumani 3 Uturuki.

https://p.dw.com/p/EcOX

Ujerumani inaendelea na juhudi za kuwakomboa wajerumani 3 waliotekwanyara nchini Uturuki.Tangu wiki iliopita wapandamilima hao wameanguka mateka wa watekanyara wa chama cha kigaidi cha kikurdi PKK.Katika kisa kingine,taarifa zimethibitishwa za kutekwa pia nyara mainjinia 2 wa kijerumani nchini Nigeria.

Ramadhan ali na ripoti zaidi:

Kikosi cha kupambana na msukosuko huu wa kutekwanyara wajerumani hao katika wizara ya nje ya ujerumani mjini Berlin kinafanya kazi mchana na usiku.Taarifa yoyote kuhusu hatima ya mahabusu hao 3 wa kijerumani huko Uturuki inachunguzwa barabara na kufuatiliwa-asema msemaji wa wizara ya nje Jens Plötner. Hakutoa taarifa zaidi na si kuhusu kisa hicho cha Uturuki wala kile cha mainjia 2 nchini Nigeria wa kampuni la ujenzi la Berger.

Kuhusu kuachwa huru kwa wapanda milima wa kijerumani nchini Uturuki kunashughulikiwa na wanasiasa wa daraja ya juu.Hapo, msemaji wa wizara ya nje Plötner alitaja mazungumzo aliokuwa nayo Kanzela Angela Merkel ,waziri wake wa nje Frank-Walter Steinmeier na waziri-mkuu wa Uturuki Erdogan na waziri wa nje Babacan mwishoni mwa wiki mjini Paris.Plötner,aliongeza:

" Tuna mabingwa huko huko na tunaendelea na juhudi zetu tena kwa nguvu.Hali ni sawa na hiyo katika mkasa uliobadilika wa wajerumani wengine waliotekwanyara nchini Somalia .

Kule tuliko na mawasiliano ya aina mbali mbali ,tunayatumia ili kufikia ufumbuzi wa kuridhisha.

Lakini naomba muelewe kwamba kama katika kesi hii nyengine ,hatuwezi kufichua mambo hadharani ili tusije kuchafua juhudi za kuwakomboa mahabusu."

Katika taarifa isiohakikishwa rasmi mwishoni mwa wiki ilisemekana watekanyara wa wapandamilima wa kijerumani nchini uturuki yamkini wakawa makamanda wa mkoa huo wenye milima wa chama cha PKK kilichopigwa marufuku nchini Ujerumamani.

Msemaji wa wizara ya nje Plötner hakudhukuru chochote juu ya taarifa hii.Bingwa wa Mashariki ya kati wa Taasisi ya sayansi na siasa,Guido Steinberg, akizungumza na TV ya DW alionya :

"Ikiwa utekajinyara huu umeandaliwa kweli na uongozi wa PKK,basi hii ni ishara ya mkondo mpya -mkondo wa kuueneza mzozo huu kimataifa.

Hatahivyo, hii ishara ya kwanza ya mtindo huo.Inapasa kwahivyo, kuchukua hadharai katika kutafsiri kitendo hiki kina maana gani.Chama cha PKK ,kina nguvu mno nchini Ujerumani.Ujerumani ni shina muhimu tangu la kukimbilia hata la kuandaa mipango ya chama hicho."

Hivi sasa kuna mabishano nchini Ujerumani iwapo wapandamilima hao kutoka Bavaria makusudi walifanya dharau hata kubidi kutiwa nguvuni.

Waziri wa ndani wa Bavaria Joachim Herrmann,alikanusha taarifa zilizochomoza katika kituo cha TV cha NTV-N24 kuwa Idara ya uhalifu ya Ujerumani ilikwisha arifu serikali juu ya hatari ziliopo hata kabla utekajinyara.