1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kuundwa kwa Serikali ya Mseto Visiwani Zanzibar

1 Februari 2010

Hatimaye Baraza la wawakilishi Zanzibar limekubaliana kuundwa kwa serikali ya umoja wa taifa.

https://p.dw.com/p/LoNw

Baada ya vuta N'kuvute, baraza la wawakilishi Visiwani Zanzibar, huko Tanzania, limekubaliana na hoja iliowasilishwa barazani na kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha CUF katika baraza hilo, Aboubakar Khamis Bakary, kutaka kufanyike marekebisho ya katiba ya serikali ya Zanzibar yatakayopelekea kuundwa serikali ya umoja wa taifa na pia kuwashirikisha wananchi, kupitia kura ya maoni, katika kuamua juu ya jambo hilo. Hii inafuatia maridhiano yaliofikiwa karibuni baina ya rais wa Zanzibar, Amani Karume , na katibu mkuu wa Chama cha CUF, Maalim Seif Shariff Hamad, ya kuukomesha uhasama wa kisiasa uliokuweko baina ya chama tawala cha CCM na CUF visiwani humo.

Othman Miraji, punde baada ya kupitishwa hoja hiyo kwenye Baraza la wawakilishi, alimuuliza kwa njia ya simu Bwana Aboubakar Khamis Bakary, vipi anavojihisi:

Mwandishi: Othman Miraji

Mpitiaji: Grace Kabogo