1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kwa nini Bunge la Tanzania lilipitisha Mswaada kuhusu Katiba Mpya?

23 Novemba 2011

Katikati ya mwezi Novemba 2011, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha Muswaada wa Uundwaji wa Tume ya Kusimamia Ukusanyaji wa Maoni ya Katiba Mpya, licha ya upinzani mkali kutoka makundi ya wanaharakati.

https://p.dw.com/p/RxwK
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Maoni Mbele ya Meza ya Duara inazungumzia hoja na mantiki za kupitishwa na kupingwa kwa Muswaada huu. Mohammed Abdulrahman amewaalika mwandishi Hawra Shamte kutoka Dar es Salaam, mwanasheria Awadh Said akiwa kisiwani Pemba, mwakilishi Hamza Hassan akiwa kisiwani Unguja na mwanaharakati wa haki za binaadamu wa Kenya, Hassan Omar.