1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kyrgyzstan waanza siku ya kwanza ya maombolezo

17 Juni 2010

Wasiwasi wazuka juu ya uwezekano wa kuzuka kwa vikundi vya itikadi kali

https://p.dw.com/p/Nt4s
Madaktari katika jimbo la Osh wakiendelea kutoa huduma kwa majeruhi wa vita vya kikabila vinavyoendeleaPicha: AP

Ikiwa leo ni siku ya kwanza kati ya siku tatu za maombolezi kufuatia machafuko yaliyosababisha mauaji ya wananchi kadhaa nchini Kyrgzstan,kumezuka kitisho kipya cha kuwepo kwa makundi yenye itikadi kali katika maeneo nchi hiyo,Kaskazini mwa mpaka na Afghanistan.

Mjumbe wa tume maalumu ya Umoja wa mataifa Miroslav Jenca ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa kuna dalili za wazi za kuzuka kwa kitisho cha makundi yenye itikadi kali katika maeneo ya bonde la Ferghana,lililopo mpakani mwa Afghanistan na Kyrgyzstan,iwapo hali ya machafuko isipodhibitiwa nchini humo.

Mjumbe huyo amefahamisha zaidi kuwa tafiti zinathibitisha kuwepo kwa vikundi kadhaa vyenye itikadi kali katika ukanda huo unaokaribiana na Uzbekistan,likiwemo kundi la Hizb ut-Tahrir,hali inayoelezewa kutishia uwezekano wa zoezi la kura ya maoni juu ya mabadiliko ya katiba nchini Kyrgyzstan, baadae mwezi huu.

Wakati hali ikielezwa kuwa inaweza kuwa mbaya zaidi kamishna wa umoja wa mataifa anayeshughulikia kitengo cha wakimbizi Antonio Guterres,ameeleza kuwa idadi ya wakimbizi wanaokimbia nchini humo inazidi kuongezeka,ambapo amearifu kuwa zaidi ya watu 3,000,waligunduliwa wakiwa wamejificha katika jengo mojawapo katika jimbo la Osh.

Kwa mujibu wa taarifa hizo,imeelezwa kuwa nchi jirani ya Uzbekistan nayo imepokea zaidi ya wakimbizi 100,000,kufuatia vita vya makabila baina ya Wakirgyzi na wauzbeki,ambapo nchi hiyo imekataa kuwapokea majeruhi na wagonjwa,hali inayowaacha maelfu ya watu kukosa msaada.

Licha ya jitihada zinazofanywa za kusambaza vyakula vya misaada kwa ajili ya wahanga wa machafuko hayo,katika kijiji kimojawapo cha Shark,baadhi ya wananchi waliobaki maeneo hayo,wamekuwa wakishutumu upendeleo unaofanywa na serikali ya muda nchini humo,kuwagawia vyakula hivyo watu wa kabila la Kyrgyz.

Machafuko hayo yanaelezwa kuwa ni mabaya zaidi kuwahi kutokea katika vita inayohusisha makabila,ambapo wahuzbeki wanatajwa kuwa ni zaidi ya asilimia 14 ya watu milioni 5.3 ya Kyrgyzstan,hali ambayo imeyalazimu mashirika ya misaada kujikuta katika wakati mgumu katika zoezi la ugawaji wa vyakula vya misaada.

Serikali ya muda ya nchi hiyo iliyomuondosha madarakani Rais

Kurmanbek Bakiyev,imeeleza kuwa jamii ya kimataifa imejiweka kando na kuiachia ikiakabiliana na matatizo ya kuwadhibiti waasi nchini humo,wanaomuunga mkono mkono Rais huyo aliye uhamishoni.

Mwandishi; Ramadhan Tuwa/DPAE/AFPE

Mhariri: Abdul-Rahman