1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lahti, Finnland. Viongozi wa Umoja wa Ulaya kukutana na Putin.

20 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD0n

Viongozi wa umoja wa Ulaya wanakutana mjini Lahti nchini Finnland kwa mazungumzo yanayotatarajiwa kulenga katika uchafuzi wa mazingira, kuzidi kwa hali ya ujoto duniani na usalama .

Rais wa bunge la Ulaya Joseph Borrell ameonya hata hivyo kutobadilisha haki za binadamu kwa gesi ya Russia.

Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair amekuwa leo akitafuta kuungwa mkono na mataifa hayo ya umoja wa Ulaya ili kuchukua hatua kali dhidi ya serikali ya Sudan kuhusiana na jimbo la Darfur, akitafuta njia nyingine za kuiwekea mbinyo , ili kuweza kukubali jeshi la umoja wa mataifa la kulinda amani katika jimbo hilo.

Blair amekuwa akikutana na viongozi wa umoja wa Ulaya katika mkutano mjini Lahti , kusini mwa Finnland, ambapo rais wa Russia Vladmir Putin amealikwa na viongozi hao na atakula nao chakula cha usiku leo.