1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Leicester City yaendelea kufanya maajabu

4 Aprili 2016

Leicester City wametanua uongozi wao kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Kandanda ya England kwa pengo la pointi saba baada ya kuwabwaga Southampton bao moja sifuri katika uwanja wa King Power

https://p.dw.com/p/1IPGD
Fußball Manchester United gegen Leicester City Barclays Premier League
Picha: Getty Images/L. Griffiths

Kocha wao Claudio Ranieri amesema kuwa “wanaiendeleza ndoto yao” bila shaka akimaanisha kulitwaa kombe la Premier League msimu huu. Leicester ina pointi 69 kukiwa na mechi sita msimu kukamilika, pointi saba mbele ya nambari mbili Tottenham Hotspur, ambao wallitoka sare ya moja moja na Liverpool Jumamosi.

Arsenal ilibakia katika nafasi ya nne, ikiwa na pointi 58 baada ya kuirarua Watford nne bila huku Manchester City ikisalia ya nne na pointi 54 baada ya kuibambua Bournemouth nne bila. Manchester United nayo inaendelea kuwinda tikiti ya kumaliza katika nne bora wakati iliifunga Everton moja bila na kusonga hadi pointi 53.

Arsenal, City na United zote zina mchezo mmoja wa ziada lakini ikiwa Leicester itashinda mechi zake nne kati ya sita zilizosalia, haiwezi kufikiwa na itakamilisha mojawapo ya hadithi za kushangaza kabisa katika historia ya 128 ya ligi ya kandanda ya England.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/reuters
Mhariri:Yusuf Saumu