1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lekerkusen yatamba katika michuano ya Ulaya

18 Februari 2011

Bayer Levekusen imetamba ugenini katika michuano ya kombe la Ulaya kwa kuikandika Metalist Kharkiv ya Ukraine mabao 4-0

https://p.dw.com/p/10JY4
Wachezaji wa Leverkusen Renato Augusto, Michal Kadlec na Hanno Balitsch wakishangilia moja kati ya mabao 4 waliyofunga dhidi ya FC Metalist KharkivPicha: picture-alliance/dpa

Yalikuwa ni mabao ya Eren Derdiyok,Gonzalo Castro na Sidney Sam aliyepachika mawili, yaliyoipatia ushindi mzito Leverkusen na kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele.

Katika mechi nyingine za michuano hiyo ya kombe la Ulaya, timu nyingine ya Ujerumani, Stuttgart, ilichapwa mabao 2-1 na Benfica ya Ureno mjini Benfica.

Stuttgart ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Martin Harnik, kabla ya Benfica kusawazisha na kuongeza la pili. Hata hivyo, bao hilo la ugenini linaiweka katika nafasi nzuri Stuttgart ya kusonga mbele.

Ama Liverpool ilitoka suluhu bin suluhu na Sparta Prague mjini Prague, matokeo kama hayo pia yakijitokeza katika mechi kati ya Napoli ya Italia na Villarreal.

Mwandishi:Aboubakary Liongo/Reuters

Mhariri:Othman Miraji