1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Leo ni siku ya Muungano Ujerumani

2 Oktoba 2012

Leo(03.10.2012)ni siku ya muungano kati ya iliyokuwa Ujerumani ya mashariki na magharibi. Miaka 22 baada ya muungano wa Ujerumani tofauti kati ya pande hizo mbili mashariki na magharibi imezidi kuwa kubwa.

https://p.dw.com/p/16J2L
Drei in Schwarz, Rot und Gelb gekleidete Figuren gehen am Samstag (02.10.1999) während des Bürgerfests zum Tag der deutschen Einheit am 3. Oktober durch die Wiesbadener Innenstadt. Unter dem Motto "Gemeinsam leben - gemeinsam feiern" begehen die Hessen und tausende von Gästen aus Deutschland und Europa zwei Tage lang den Geburtstag des einheitlichen deutschen Staates. Hessen hat derzeit die Präsidentschaft im Bundesrat inne und richtet damit das Fest aus. dpa/lhe (Digitale Fotografie)
Ishara ya muungano, raia wamejipaka rangi ya bendera ya Ujerumani mojaPicha: picture-alliance/dpa

Pato jumla la mwaka katika Ujerumani ya mashariki limepungua kwa asilimia mbili na linafikia sasa asilimia 71 chini ya kiwango cha upande ndugu zao wa magharibi. Matarajio hata hivyo yanaonekana kuwa mabaya zaidi.

Vijana wanahama kutoka maeneo hayo, na kusababisha kukosekana kwa nguvu kazi ya vijana katika soko la kazi la upande wa mashariki. Mishahara na mapato yako chini kwa theluthi moja ukilinganisha na upande wa magharibi.

Lakini hata upande wa magharibi, eneo lote linapambana na matokeo ya mabadiliko ya mfumo, hasa katika eneo la Ruhr kwa mfano. Baada ya shauku kubwa ya muungano hivi sasa hali imerudi chini kidogo.

Mwanzoni kulikuwa na hali ya amani na kisha likapanda joto la shauku. Ni hali ya kibinadamu, ambapo uzoefu huu alilazimika kiongozi wa wakati huo wa iliyokuwa Ujerumani ya zamani Erich Honecker kuishi nayo katika mwaka 1989.

ARCHIV - Der Staats- und Parteichef der DDR, Erich Honecker, aufgenommen am 8. Oktober 1989 während der Feierlichkeiten anlässlich des 40-jährigen Bestehens der DDR. Honecker verdankte seinen Aufstieg einer "lupenreinen proletarischen Vergangenheit", seinem Gespür und nicht zuletzt seinem Vorgänger Ulbricht, den er 1971 mit der Billigung Moskaus stürzte. Foto: Wolfgang Kumm dpa/lbn (zu "Honecker: Ein Leben für den Kommunismus" vom 13.10.2009) +++(c) dpa - Bildfunk+++
Kiongozi wa iliyokuwa Ujerumani mashariki DDR Erich Honecker 1989Picha: picture-alliance/dpa

Kiongozi huyo wa Ujerumani mashariki alitoa tathmini mwezi Januari mwaka huo ambapo miezi kumi baadaye alikuja kutambua kuwa ni kosa kubwa alilolifanya. Honecker alikuwa na wasi wasi juu ya hali ya baadaye ya ukuta wa Berlin.

Alitaka ukuta huo ubakie kama ulivyo katika muda wa miaka 50 au hata 100 ijayo, iwapo sababu ya kuondolewa kwa ukuta huo haikupatikana, aliamini kiongozi huyo wa DDR.

Kikwazo cha kuondolewa ukuta

Kikwazo kikubwa cha kuondolewa kwa ukuta huo unaouzuwia ufashisti kwa mtazamo wake ni ubepari. Kuna hali bado iliyopo katika uchumi wa masoko iliyothibitika kuwa una uwezo wa kufanyakazi katika hali ya mbinyo na pia kuwa na jamii iliyo na uwezo wa kuhurumiana.

BRD: Honecker-Besuch Nach der Begrüßung des Generalsekretärs des ZK der SED und Vorsitzenden des Staatsrates der DDR Erich Honecker, durch den Bundeskanzler Helmut Kohl vor dem Bundeskanzleramt in Bonn erklangen die Hymnen der beiden deutschen Staaten. Datierung: 7. September 1987 Fotograf: Oberst, Klaus Quelle: Bundesarchiv
Erich Honecker akiwa na kiongozi aliyeongoza muungano kutoka Ujerumani magharibi Helmut Kohl mwaka 1987Picha: Bundesarchiv - Bild 183-1987-0907-017

Kama sio hali ya kuwa na madaraka ya kupita kiasi katika uchumi wa kupangilia, Ujerumani mashariki pia ingekuwa kama hivyo.

Ni hali hiyo na utendaji usiokuwa na mfano ndivyo vinavyotenganisha karibu miaka 44 ya mtengano wa nchi hizo ambao unapaswa kuwekwa sawa. Katika hali hiyo kumefanyika pia makosa. Hali iliyoleta tofauti hii inayoonekana. Cha muhimu hapa ni kwamba watu wa Ujerumani mashariki binafsi wameamua kupambana na serikali inayowakandamiza, na kuweza kupata kujikomboa na kuleta muungano.

Kama sharti , kwanza yalipatikana makubaliano katika bunge la Ujerumani mashariki , lililokaa August 23, 1990, na kuingiza kifungu ambacho kitaitambua Ujerumani mashariki , kifungu ambacho kitaingizwa katika katiba ya Ujerumani magharibi , ambacho ni ibara ya 23 ya katiba ya Ujerumani magharibi.

Siku ya muungano Oktoba 3, mwaka 1990 ilikuwa ni siku ya mabadiko yaliyoingiza hamasa kubwa kwa Wajerumani. Katika mwaka wa mwisho wa kuwapo kwake, Ujerumani mashariki, maarufu kama DDR, jamhuri hii ya kidemokrasi ya Ujerumani haikuwa kama ilivyokuwa hapo zamani.

Bidhaa za DDR

Kansela wa zamani Willi Brandt, aliwahi kusema kuwa vitu vinavyohusiana , kisiasa kijiografia na kijamii ni lazima vikue kwa pamoja.

Various graffiti are painted on the Berlin Wall on the West Berlin side on April 29, 1984. The Berlin wall built by the East German government to seal off East Berlin from the part of the city occupied by the three main western powers (USA, Great Britain and France), and to prevent mass illegal emigration to the West. The wall, built along the border between German Democratic Republic (GDR) and Federal Republic of Germany, was the scene of the shooting of many East Germans who tried to escape from GDR. The two countries remained divided until November 1989 when the wall was unexpectedly opened following increased pressure for political reform in GDR. (Photo credit should read JOEL ROBINE/AFP/Getty Images)
Ukuta wa Berlin mwaka 1984Picha: AFP/Getty Images

Uchumi hauendi kwa pamoja. Viwanda vilivyokuwa upande wa mashariki havikuwa na viwango vya kimataifa. Kumekuwa na harakati nyingi , uzalishaji ulikuwa mdogo, ubora wa bidhaa uko chini ya ule wa bidhaa kutoka upande wa magharibi. Tume maalum iliyoundwa baada ya muungano, Treuhand, iliweza kuyauza karibu mashirika 14,000 ya serikali.

Ujerumani ya mashariki ilijikuta katika hali ya kuuzwa. Kwa mkataba wa mshikamano , mpango mkubwa wa kwa ajili ya upande wa mashariki ulianzishwa , na kuingiza kati ya mwaka 1990 hadi 2010 kiasi cha euro bilioni 1.4 katika iliyokuwa Ujerumani ya mashariki.

Karibu theluthi mbili ya fedha hizo imekwenda kwa mafao ya jamii. Mkataba huo wa kihistoria unakwenda hadi mwaka 2019. Hadi mwaka huo mahitaji ya eneo hilo la mashariki yanapungua ngazi kwa ngazi kila mwaka.

Mwandishi: Marcel Fürstenau / ZR/ Sekione Kitojo

Mhariri: Mohammed Khelef.