1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Leo ni zamu ya Kombe la UEFA

17 Septemba 2009

champions League-mabingwa Barcelona hawakutamba

https://p.dw.com/p/Jj2X
Grafite atamba tena.Picha: AP

Baada ya duru ya kwanza jana usiku ya champions League-kombe la klabu bingwa barani ulaya kumalizika,leo ni zami ya Kombe la pili la ulaya-kombe la UEFA:Ujerumani inawakilishwa na timu 2 za kaskazini:Hamburg yenye miadi leo huko Austria na Rapid Vienna na Bremen ilioitembelea Funchal.Lakini, macho na masikio ya mashabiki yalikodolewa Kombe la klabu bingwa-champions league na hasa mpambano kati ya mabingwa FC Barcelona ya Spian na Inter Milan, mabingwa wa Itali.

Mabingwa FC barcelona walianza kutetea taji lao kwa kutoka sare tu 0:0 na wenyeji wao Inter Milan wakati Arsenal ya Uingereza ilitoka nyuma kwa m abao 2 na mwishoe kuwambia wabelgiji Standard Liege-kutangulia si kufika.Waakilishi wa ujerumani Stuttgart pia hawakufua dafu nyumbani,kwani waskochi Glasgow rangers waliondoka na pointi 1 .Ilikua Rangers iliolifumania kwanza lango la Stuttgart hadi pale dakika ya 77 ya mchezo Madjid Bougherra aliposawazisha kwa Stuttgart.Pavel Pogrebnyak ndie aliewapatia waskochi bao lao.

Mabingwa FC Barcelona, walidhibiti zaidi dimba uwanjani San Siro na mapema mswede Ibrahimovic nusra atie bao langoni mwa Inter Milan -klabu yake ya zamani.Lakini mwishoe, si yeye wala mkamerun Samuel Eto-o -jogoo la zamani la Barcelona aliewika.

Mshambulizi wa danmark Nicklas Bentner aliipatia Arsenal bao lake la kwanza muda mfupi kabla kipindi cha mapumziko na mabao ya dakika za mwisho kutoka Thomas Vermaelen na eduardo yaligeuza mkondo wa mchezo.Ingawa Standard Liege ililalamika bao la dakika ya 78 la Vermaelen lililosawazisha, hatima ya wabelgiji ilikuwa imeshakatwa .Halafu Eduardo akaupiga msumari wa mwisho katika jeneza lao kwa bao la 3.Dynamo Kiev ya Ukraine, iliwalaza mabingwa wa Urusi Rubin Kazan kwa mabao 3-1.

Wagiriki Olympiakos pia wamefurahia ushindi kufuatia bao la Vassilis Torosidis katika lango la Alkamaar.Mshambulizi wa Itali Alberto Girladino, alitolewa nje ya uwanja na rifu kwa kadi nyekundu kwa kupiga kisugudi huko Fiorentina na kusababisha pigo la bao 1:0 kutoka Olympique Lyon.Baada ya duru hii ya Kombe la UEFA, kesho Bundesliga yarudi uwanjani:

Mabingwa Wolfsburg wana miadi na kocha wao wa zamani aliewatawaza mabingwa Felix Magath huko Gelsenkirchen- nyumbani kwa Schalke.Wolfsburg ilianza juzi uzuri kampeni yake katika champions league pale mbrazile Grafite, alipoirarua CSKA Moscow kwa hattrick-mabao 3 -1.Ingawa Wolfsburg haikuanza uzuri msimu huu wa Bundesliga, Grafite anadai, mashini yao sasa imeshapata moto na kesho Felix Magath atajuta kwanini aliihama Wolfsburg kuhamia Schalke .Schalke ikinyatia nafasi ya 3 ya ngazi ya ligi ,haitataka kuteremka na kumuaibisha kocha wao mpya.

Mwandishi:Ali Ramadhan /rtr/afp/dpa

Mhariri:M.Abdul-Rahman