1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Leverkusen yampa mkataba mpya Henrichs

17 Mei 2017

Bayer Leverkusen wamempa mkataba mpya wa miaka miwili beki chipukizi katika timu ya  taifa ya Ujerumani Benjamin Henrichs, na sasa atasalia katika klabu hiyo hadi mwaka 2022.

https://p.dw.com/p/2d7CK
Fußball Benjamin Henrichs
DFB U21 Nationalmannschaft, 
Deutschland - Slowakei
Benjamin HenrichsPicha: picture-alliance/augenklick/firo Sportphoto

Haya ni kwa mujibu wa klabu hiyo ya ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga.

Henrichs mwenye umri wa miaka 20 alijiunga na Leverkusen akiwa mdogo na alicheza mechi yake ya kwanza katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo Septemba 2015. Ameichezea timu ya taifa ya Ujerumani mechi moja pekeyake na ilikuwa dhidi ya San Marino mwezi Novemba mwaka 2016.

Mkataba wake wa awali ulikuwa unakamilika mwaka 2020 na sasa kulingana na duru, mkataba huu mpya umeshuhudia mchezaji huyo kuongezwa mshahara.

1. Bundesliga 33. Spieltag | SV Darmstadt vs. Hertha BSC
Jerome Gondorf katikati amesajiliwa na Werder Bremen kutoka DarmstadtPicha: Getty Images/AFP/D. Roland

"Ninafuraha sana kwa kuwa nimeweza kuwa mchezaji wa kulipwa na nimeweza pia kuichezea timu ya taifa nikiwa Bayer. Baada ya msimu uliokuwa mgumu, nataka kuisaidia klabu hii irudi katika kile kiwango chake cha mchezo," Henrichs alisema katika taarifa.

Leverkusen wamekuwa na msimu mbovu kulingana na kiwango chao, kwani wanaorodheshwa katika nafasi ya 12 katika Bundesliga, mbele ya mechi yao ya kufunga msimu Jumamosi watakapokwaana na Hertha Berlin ugenini. Huku hayo yakiarifiwa, klabu ya Werder Bremen imesema inatarajia kumsajili kiungo Jerome Gondorf wa klabu iliyoshuka daraja ya Darmstadt. Usajili  wa Gondorf utakuwa wa pili kwa Bremen ambayo kwasasa iko katika nafasi za katikati katika jedwali la ligi kuu ya Ujerumani, na hii ni baada ya kumsajili beki wa kushoto wa  Sweden Ludwig Augustinsson kutoka Copenhagen ya Denmark.

Bremen hawakutoa taarifa zaidi, walilosema ni kwamba Gondorf amepita uchunguzi wa kiafya na kwamaba atatia saini mkataba hivi karibuni.

Mwandishi: Jacob Safari/DPAE

Mhariri: Sekione Kitojo