1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LEVI: Mawaziri wa ulinzi wa Umoja wa Ulaya kujadili kikosi cha Kongo

2 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD71

Mawaziri wa ulinzi wa Umoja wa Ulaya watajadili kikosi cha kulinda amani kilicho nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Shinikizo linazidi la kukitaka kikosi hicho kiendelee kubakia baada ya duru ya pili ya uchaguzi mnamo Oktoba 29, huku ikihofiwa huenda kukazuka machafuko.

Jeshi la Umoja wa Ulaya limepangiwa kuondoka Kongo Disemba mosi baada ya matokeo rasmi ya duru ya pili ya uchaguzi kutangazwa.

Mawaziri hao watakaokutana kaskazini mwa Finland watajadili pia juu ya hali ya jimbo la Kosovo na mpatanishi wa Umoja wa Mataifa, Martti Ahtsaari. Umoja wa Ulaya una jukumu kubwa katika jimbo hilo la Kosovo.