Liberia: Boakai akubali kushindwa na Weah

Makamu wa rais wa Liberia Joseph Boakai amekubali kushindwa katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais na nyota wa zamani wa soka George Weah

Makamu wa rais wa Liberia Joseph Boakai amekubali kushindwa katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais dhidi ya nyota wa zamani wa soka George Weah, na kurahisisha mchakato wa nchi hiyo kuelekea makabidhiano yake ya kwanza ya madaraka kidemokrasia katika miongo kadhaa.

Kukubali kushindwa kwa Boakai kunaepusha changamoto za kisheria zilizofuatia baada ya duru ya kwanza ya uchaguzi na kuchelewesha duru ya pili kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Weah atamrithi Ellen Johnson Sirleaf kama rais mwezi ujao. Matokeo ya awali yameonyesha kuwa Weah amejipatia asilimia 61.5 ya kura, baada ya kuhesabiwa kwa zaidi ya asilimia 98 ya kura.

Hata hivyo nyota huyo wa zamani wa kandanda aliyewahi kuzichezea klabu za AC Milan, na Paris Saint Germain anakabiliwa na kibarua kigumu katika serikali yake baada ya kampeni ambamo alitoa mapendekezo kidogo kuhusu sera makhsusi.

Maudhui Zinazofanana

Matukio ya Afrika | 29.12.2017

George Weah ashinda uchaguzi wa rais Liberia

Matukio ya Afrika | 26.12.2017

Waliberia wamchagua rais

Mada Zinazohusiana

Tufuatilie