1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ligi ya Mataifa ya UIaya yaonyesha mafanikio

Bruce Amani
21 Novemba 2018

Hatua ya Makundi ya Kinyang'anyiro cha kwanza kabisa cha Ligi ya Mataifa ya Ulaya – UEFA Nations League, imekamilika na licha ya kutiliwa shaka, tamasha hilo linaonekana kuimarisha kandanda la Ulaya.

https://p.dw.com/p/38fth
Logo UEFA Nations League
Picha: picture-alliance/dpa/UEFA

Mashindano hayo ya kwanza kabisa kuwahi kuandaliwa yanaonekana kupata mafanikio ya mapema lakini baada ya kukamilika awamu ya makundi, nchi zilizonufaika zaidi ni zinazoangazia mashindano ya Euro 2020.

Wakati Uholanzi, England, Uswisi na Ureno zikiandaa kushiriki fainali za Ligi ya Mataifa Juni 2019, ni mashindano ya Ulaya ya Euro yatakayoandaliwa mwaka mmoja baadaye ambayo yalikuwa na faida kubwa.

Moja kati ya timu ndogo za Georgia, Macedonia, Kosovo au Belarus itajihakikishia tikiti ya kutinga fainali za Euro zenye nchi wanashiriki 24 baada ya zote kupata nafasi ya kucheza mechi ya mchujo kwa kushinda makundi yao katika ngazi ya chini kabisa ya League D.

Katika League C, ushindi wa Scotland huenda ukawa ni hatua ya kwanza kurejea katika fainali kuu, huku ikiangazia Zaidi mkondo wa kuelekea Euro 2020 na sio hata kupandishwa daraja hadi League B.

"Ligi ya Mataifa ilikuwa na hata imefanikiwa Zaidi kuliko tulivyodhani,”. Amesema Aleksander Ceferen, rais wa Shirikisho la Kandand Ulaya – UEFA.

Fußball UEFA Nations League Deutschland vs. Niederlande | Jogi Löw
Ujerumani lazima ijipande upya baada ya kushushwa darajaPicha: Getty Images/AFP/P. Stollarz

Ceferen amesema sio tu kukamilika kwake ndiko "kulikofurahisha zaidi" bali kulitoa "mkondo wa kundi D kufuzu katika michuano ya Euro. Haingwezekana kwa urahisi hapo kabla.”

Kauli hiyo ni kinyume na ya baadhi ya watu wanaopuuzulia mbali mashindano hayo, kama vile kocha wa zamani wa Ujerumani Berti Vogts ambaye ametoa uondolewe "maramoja.”

Gazeti la Ujerumani la Sueddeutsche Zeitung lilikuwa na maoni mazuri lakini linaamini kuwa hali halisi ya kinyang'anyiro hicho cha karibuni bado haijulikani.

Hakika, michuano ijayo itakayoanza mwishoni mwa mwaka wa 2020, huenda ikaathirika kwa sababu haijafahamika kama kutatolewa nafasi ya mechi za mchujo kwa ajili ya Kombe la Dunia. Na kama sio hivyo, hilo huenda hata likahimiza kushushwa daraja hadi ligi dhaifu kwa 2022 – wakati mechi za mchujo za kuwania nafasi za Euro 2024 zitakapotolewa.

Mabingwa mara nne wa dunia Ujerumani lazima wakabiliwe na fedheha ya kushushwa daraja na kuukamilisha mwaka wao mbovu wa 2018 wakati England ikilenga kutwaa taji la kwanza kuu tangu 1966. 

Timu nne za Nations League zitacheza nchini Ureno huku nusu fainali ikiwa Juni 5-6, 2019 na fainali ikichezwa Juni 9 ili kujua mshindi wa kwanza kabisa wa Ligi ya Mataifa – UEFA Nations League!

Mwandishi: Bruce Amani/DPA
Mhariri: Iddi Sessanga