1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LIMA: Tetemeko la ardhi limeua watu 450 nchini Peru

17 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBYV

Si chini ya watu 450 wameuawa katika tetemeko la ardhi lililotokea nchini Peru.Zaidi ya watu 1,500 pia wamejeruhiwa.Tetemeko lililokuwa na nguvu ya 7.9 kwenye Kipimo cha Richter,ni baya kabisa kupata kutokea nchini humo tangu miaka 27 iliyopita.Kiini cha tetemeko lililoteketeza maelfu ya nyumba,kilikuwa baharini umbali wa kama kilomita 148 kusini ya mji mkuu,Lima.

Serikali ya Peru imetangaza hali ya hatari.Wakati huo huo katika hatua ya tahadhari,watu wengine wameondoshwa kwenye nyumba zao na wamepiga kambi barabarani.